Polisi nchini Kenya imetangaza kuwatambuwa rasmi wanafunzi saba wanaoshukiwa wakuu wa uchomaji moto wa bweni katika shule ya wasichana wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapilli (Mei 31) 2026 na polisi, imetaja idadi ya wanafunzi saba ambao hawakutaja majina, wamegundulika baada ya kupatikana picha za kamera ya usalama.
Tukio hilo la kuungua kwa bweni la wasichana katika shule ya Utumishi nchini Kenya lilitokea usiku wa Jumatano kuamkia Alhamis, ambapo wanafunzi 16 walipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Moto huo ulianza kwenye ghorofa ya kwanza ya bweni hilo, ambayo kwa ujumla ilikuwa na vitanda 135, kwa mujibu wa polisi.
(Feed generated with FetchRSS)