WHO imesema zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili, huku wengi wakikosa huduma stahiki.

Mwongozo huo unatoa maelekezo ya jinsi ya kuanzisha na kutekeleza huduma za msaada,zikiwemo zinazotolewa kwa njia za kidijitali au kwa msaada wa wahudumu wasio wataalamu lakini waliopata mafunzo.

Mbinu za huduma za afya ya akili

Shirika hilo linaeleza kuwa mbinu hizo zimeonesha mafanikio katika kupunguza dalili za msongo wa mawazo na wasiwasi, hasa katika maeneo yenye rasilimali chache na yaliyoathiriwa na migogoro.

Mwongozo huo pia unaelekeza utekelezaji wa hatua mbili za matibabu za WHO,  wa “Step-by-Step” au Hatua kwa Hatua na “Doing What Matters in Times of Stress”  au “Kufanya Yaliyo Muhimu Wakati wa Msongo wa Mawazo”, ambazo tayari zinatumika katika huduma za kitaifa nchini Lebanon na Thailand.

WHO inaamini kuwa mwongozo huu utachangia juhudi za kimataifa za kupanua wigo wa huduma za afya ya akili zinazopatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *