
Nchini Madagascar, mashauriano ya kitaifa, yaliyoahirishwa mara kwa mara tangu mwanzo wa mwaka, yamesogezwa mbele tena mnamo Juni 3. Kanali Michaël Randrianirina, rais wa sasa wa Madagascar, alitumia fursa ya siku hii, ambayo ilitakiwa kuwa siku ya uzinduzi, kutangaza rasmi jukumu kuu la Baraza la Kiekumeni la Makanisa ya Kikristo katika mchakato ujao.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Antananarivo, Aurélie Kouman
“Tutafute manufaa zaidi ya Taifa hapa. Hakutakuwa na hesabu au ubinafsi, kwa sababu mustakabali wa Madagaska unategemea mkutano huu!” Ilikuwa kwa maneno haya ambapo Rais wa Ufufuo alikutana na Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, washauri wawili wakuu, na wakuu wanne wa makanisa ya Kikristo mnamo Juni 3, 2026.
Kufuatia mkutano huu, Kanali Michaël Randrianirina alithibitisha rasmi kile alichokuwa akitetea kwa wiki kadhaa: Fiombonan’ny Fiangonana Kristiana eto Madagasikara (FFKM, Baraza la Kiekumeni la Makanisa ya Kikristo) litaongoza mashauriano ya kitaifa. Wizara ya yenye dhmana ya Mipango na Uwekezaji itakuwa na jukumu la kusaidia makanisa katika masuala ya kiufundi, vifaa, na kifedha, kuanzia ngazi ya chini hadi nchi nzima.
Mvutano kati ya Makanisa ya Kikristo na Wizara ya Mipango ya Nchi
Kwenye karatasi, hii inaashiria mwisho wa uhasama wa muda mrefu. Kwa miezi kadhaa, mvutano ulikuwa ukiongezeka kati ya viongozi wa kidini na wizara hii. Viongozi wa kanisa walilalamika kuona wanatengwa hatua kwa hatua kutoka kwa mchakato huo.
Kwa sasa, FFKM haijazungumza chochote kuhusu mkutano huo. Mkutano na waandishi wa habari unatarajiwa katika siku zijazo ili kufafanua ratiba. Jambo moja nyeti linasalia: FFKM inatetea mashauriano marefu, kuanzia na uchaguzi wa serikali za mitaa, ilhali baadhi ya watu walio karibu na serikali wanashinikiza uchaguzi wa urais wa haraka