Kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika hilo huko Geneva, Uswisi watoto hao wadogo, ambao ni asilimia 9 tu ya idadi ya watu duniani, wanachangia karibu theluthi moja ya magonjwa yote yanayosababishwa na chakula. Magonjwa ya kuhara yanatajwa kuwa miongoni mwa yanayoua zaidi kundi hilo la watoto.

WHO imeeleza kuwa uchafuzi wa chakula unaotokana na bakteria, virusi na vimelea vingine ulisababisha wagonjwa wapatao milioni 860 mwaka 2021. Aidha, kemikali hatari zilichangia asilimia 73 ya vifo vyote vinavyohusishwa na chakula kilichochafuliwa.

WHO imetoa ripoti hii ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Chakula duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 7 na mwaka huu, inakuja na kaulimbiu Kutoka mzigo hadi suluhisho chakula salama kila mahali.”

Nchi zinawajibu

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema usalama wa chakula si suala la kinadharia bali linagusa kila mlo na kila familia kila siku.

“Kwa mara ya kwanza, nchi zina takwimu zao za kuona maeneo yenye mzigo mkubwa zaidi wa magonjwa yanayotokana na chakula. Maarifa hayo yatazisaidia serikali kuweka vipaumbele vya hatua zinazohitajika kulinda afya za wananchi,” amesema Dkt.Tedros.

Maeneo yanayoathirika zaidi

Ripoti hiyo inaonesha kuwa Afrika na Kusini Mashariki mwa Asia zinabeba karibu robo tatu ya wagonjwa wote wanaotokana na chakula kisicho salama na asilimia 60 ya vifo duniani.

Mbali na athari za kiafya, WHO inakadiria kuwa magonjwa hayo yalisababisha hasara ya takribani dola bilioni 310 kutokana na kupotea kwa uzalishaji kazini mwaka 2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *