MAKAMU wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ametoa maagizo 10 kwa wadau wa mazingira, ikiwamo mamlaka za Serikali za Mitaa hususan manispaa na majiji, kuanzisha bustani za kijani na kuhakikisha zinatunzwa ipasavyo.

‎Dk. Nchimbi ametoa maagizo hayo leo juni 5, 2026 jijini  Dodoma  wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan. ‎Pia, ameagiza mamlaka zinazotoa vibali vya ujenzi kuweka sharti na kusimamia ili kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiambatane na agizo la kupanda miti isiyopungua mitano.

‎‎Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Yusuf Hamad Masauni, amesema katika maadhimisho hayo mwaka huu shughuli nyingi zimefanyika za utoaji elimu ya utunzaji wa mazingira.

‎Masauni amesema programu hiyo inalenga kuchochea matokeo makubwa na ya haraka katika kurejesha uoto wa asili, kuimarisha ustawi wa mifumo ikolojia pamoja na huduma za kiikolojia ambazo ni msingi muhimu wa uzalishaji katika sekta mbalimbali za uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *