• Aliyekuwa staa wa Kenya katika timu ya taifa, Dennis Oliech, amesema alikataa KSh 890 milioni kuhama Kenya
  • Anasema ni fedha alizokataa kupokea kutokana na uzalendo wake kwa taifa la Kenya
  • Oliech kwa sasa anasema maisha yake yamebadilika na ameitaka mamlaka ya soka nchini kumpa nafasi ya kujipatia kipato

Aliyekuwa nyota wa soka nchini Dennis Oliech amefunguka kuhusu ofa kubwa aliyowahi kuikataa ya kuuza uraia wake.

Uzalendo: Oliech Alidinda Kupokea KSh 890M Kubadilisha Uraia
Aliyekuwa mchezaji hodari wa Harambee Stars Dennis Oliech wakati wa enzi yake. Picha: Dennis Oliech
Source: Facebook

Oliech alisema alipokuwa aking’aa kama mchezaji wa Harambee Stars, alipokea ofa ya KSh 890 milioni ili abadilishe uraia na kuhamia Dubai mwaka 2004.

Wakati huo akiwa na miaka 19, gazeti la Guardian la Uingereza lilimtaja kama mmoja wa vipaji vinavyosakwa zaidi, akicheza sambamba na nyota kama Wayne Rooney, Robin van Persie na Wesley Sneijder.

Oliech amesema kwa sasa anatafakari ofa hiyo kwa mtazamo tofauti na kwamba angeweza kuikubali kama ingekuja leo.

“Naweza kusema niko 50-50 kwa sababu hii leo nikipewa nitachukua, lakini wakati huo niliona ni sawa kuikataa. Nchi za Kiarabu mambo ni tofauti,” alisema katika mahojiano na Jeff Kinyanjui.

Pia soma

Magazeti ya Kenya: Matiang’i alegeza msimamo kuhusu mgombea wa urais wa upinzani

Aliongeza kuwa kama ofa hiyo ingetoka Uingereza angekubali mara moja kubadilisha uraia ili kuendeleza kipaji chake.

“Kama ingekuwa Uingereza ningekubali kubadilisha uraia wangu,” alisema.

Maisha baada ya soka ni vipi kwa Oliech?

Oliech amesema maisha baada ya soka hayajakuwa rahisi na ameomba usimamizi wa soka nchini kumpa nafasi ya kujipatia kipato, kama kocha wa vijana au nafasi nyingine.

“Maisha baada ya kandanda hayajakuwa mazuri. Ningependa kuwa kocha wa watoto au nafasi yoyote,” alisema.

Alitoa ushauri kwa wachezaji wa sasa kuwekeza mapato yao mapema.

“Usisubiri pesa nyingi. Weka biashara au nunua bodaboda mbili zikuletee kipato kidogo, itakusaidia baadaye,” alisema Oliech.

Mwanasoka huyo aliwataka wachezaji wa sasa kuwekeza wanachopata kwenye kazi au biashara zao.

“Usisubiri eti pesa nyingi, wekea bibi biashara au nunua bodaboda mbili zikuwe zikikuletea hiyo mia tatu tau, siku moja itakusaidia,” alisema Oliech.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *