• Ajali ya barabarani kwenye Barabara Kuu ya Webuye-Bungoma imegharimu maisha ya watu sita na kuwaacha wengine wakiwa wamejeruhiwa Jumatano, Juni 10
  • Mgongano huo ulihusisha matatu ya Eldoret Victory Shuttle na trela, na kusababisha maafa makubwa
  • Video kutoka eneo la tukio ilionyesha picha ya kusikitisha ya ajali hiyo, huku trela ikionekana kuisaga kabisa matatu hiyo ya abiria wa umma (PSV)

Ajali mbaya imetokea kwenye Barabara Kuu yenye shughuli nyingi ya Webuye-Bungoma, na kuacha watu kadhaa wakiwa wamefariki huku wengine wakijeruhiwa.

Ajali ya Mabanga
Majonzi Mabanga: Watu 6 Wafariki Baada ya Matatu na Lori Kugongana Kwenye Barabara ya Webuye-Bungoma
Source: Facebook

Ajali hiyo ya kutisha ilitokea majira ya saa sita usiku mnamo Jumatano, Juni 10, katika eneo la Makotelo karibu na Mabanga.

Ajali ya Mabanga ilitokeaje?

Ripoti za awali zinaonyesha kwamba ajali hiyo mbaya ilihusisha matatu ya Eldoret Victory Shuttle yenye nambari za usajili KBV 811 na trela yenye usajili KCAA 203A.

Ajali hiyo ya kutisha ilitokea baada ya matatu hiyo ya PSV kugongana uso kwa uso na trela kisha kupinduka na kuingia katika shamba la mahindi, na kuwaua watu sita papo hapo huku wengine kadhaa wakipata majeraha mabaya.

Pia soma

Aliyenusurika ajali ya Salama akumbuka maneno ya mwisho aliyotamka rafiki yake kabla ya kufariki

Mashahidi walieleza jinsi ajali hiyo ilivyokuwa ya kutisha, wakisema miili ya waliofariki ilitapakaa barabarani na ndani ya shamba la mahindi.

Video iliyoshirikiwa na Okhwa Lupa Live ilionyesha jinsi ajali hiyo ilivyokuwa mbaya, huku vitu mbalimbali vikionekana vimetapakaa eneo la tukio.

Video hiyo iliyoonekana na TUKO.co.ke ilionyesha picha ya kuhuzunisha ya ajali hiyo, huku trela ikionekana kuisaga kabisa matatu hiyo ya PSV na magari yote mawili yakiharibika vibaya.

Polisi tayari wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Kwa nini NTSA ilisimamisha Saccos nne za PSV?

Katika habari nyingine, Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) ilisimamisha leseni za waendeshaji wanne wa usafiri wa umma kufuatia msururu wa ajali mbaya za barabarani zilizorekodiwa wakati wa msimu wa sherehe za Desemba 2025.

Mamlaka hiyo ilisimamisha Saccos na kampuni kadhaa kutokana na kutofuata kwa kiwango kikubwa kanuni za usalama, ikiwemo ukiukaji unaohusiana na mwenendo wa madereva na udhibiti wa mwendo kasi.

NTSA ilitangaza Jumatatu, Januari 19, kwamba Idara ya Trafiki itakamata magari yoyote yanayoendeshwa na waendeshaji hao yatakayopatikana yakikiuka agizo la kusimamishwa kwao, na kuushauri umma kuepuka kutumia huduma zao.

Pia soma

Mvulana wa darasa la 4 aliyetumwa nyumbani kuleta ada ya KSh 100 akanyagwa na lori

Aidha, NTSA imeziagiza Saccos zilizosimamishwa kuwaondoa madereva wao katika majukumu yote ya uendeshaji na kuwasilisha magari yote yenye ukiukaji kwa wauzaji walioidhinishwa wa vifaa vya kudhibiti mwendo kasi ili vifanyiwe ukaguzi wa utendaji kazi.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *