
Fulana za michezo zenye jina la “Jezi ya Kombe la Dunia ya Hind Rajab” zimezinduliwa rasmi sambamba na mashindano ya kombe hilo yanayoendelea katika nchi za Marekani, Canada na Mexico; jezi ambazo zimebuniwa na kutengenezwa kwa idhini ya mama wa “Hind Rajab”, mtoto wa Kipalestina aliyeuawa shahidi na askari wa Israel.
Waandaaji wa mpango huo wametangaza kwamba lengo lake ni kuelekeza fikra za walimwengu kwenye hali mbali ya watu wa Ukanda wa Gaza na mateso ya watu wa Palestina.
Kwa mujibu wa waandaaji, mapato yote yatakayotokana na mauzo ya jezi hizo yatatengwa kwa ajili ya familia ya daraja la kwanza ya Hind Rajab, pamoja na mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayofanya kazi ndani ya Ukanda wa Gaza.
Tarehe 29 Januari, 2024, mtoto Hind Rajab aliyekuwa na umri wa miaka 6 alishambuliwa na vifaru vya Israel katika eneo la Tel Al-Hawa huko Gaza, akiwa pamoja na wanafamilia sita.
Hind Rajab, alinaswa kwenye gari akiwa pamoja na familia yake baada ya shambulio la anga la Israel, lakini alinusurika na kutumia zaidi ya saa moja kuwasiliana kwa simu na Hilali Nyekundu ya Palestina akiomba msaada wa kumuokoa.
Sauti yake ya kutetemeka, akisema mara kwa mara, “Ninaogopa, nataka kubakia hai,” imesajiliwa katika historia; lakini kabla ya waokoaji kumfikia, ambulensi yao ilishambuliwa kwa mabomu na timu yote ya uokoaji iliuawa kishahidi. Muda mfupi baadaye, askari wa Israel walikomesha maisha mafupi ya msichana mdogo, Hind Rajab, kwa kummiminia risasi moja kwa moja.
Maiti ya Hind Rajab aliyekuwa na umri wa miaka 6 alipatikana ndani ya gari lililokuwa limepigwa risasi 335 katika mji wa Gaza. Alikuwa ndani ya gari hilo pamoja watu sita wa familia yake ikiwa ni pamoja na mjomba, mke wake, na watoto wao watatu, ambao wote waliuawa