
Makao makuu ya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) yamefutilia mbali shutuma zinazoyahusisha na njama inayodaiwa ya kupindua utawala uliopo. Kwa siku kadhaa, jumbe zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, majukwaa ya kidijitali, na ndani ya baadhi ya makundi ya wanasiasa wamemedai jaribio lililopangwa la kuhatarisha usalama wa taifa kwa kuipindua serikali. Jeshi linaelezea taarifa hii kama ya uwongo na isiyo na msingi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa iliyochapishwa mnamo Juni 13, makao makuu ya jeshi yanalaani vikali madai haya kama ya kashfa, ya uwongo, na ni madai yasiyokuwa na msingi wowote.
Makao makuu ya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati yanadai kwamba shutuma hizi zinalenga kuchafua taswira yake na ya mkuu wake, Jenerali Zéphirin Mamadou, pamoja na kudhoofisha juhudi za kuimarisha vikosi vya wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Makao makuu ya jeshi yanabainisha tena kujitolea kwao kwa taasisi za Jamhuri, kuheshimu utaratibu wa kikatiba, na uaminifu wao kwa Rais wa Jamhuri na Amri jeshi mkuu, Faustin-Archange Touadéra.
Kutokana na kuenea kwa uvumi huu, jeshi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa macho na kujizuia ili kuepuka udanganyifu wowote unaoweza kuhatarisha utulivu wa nchi. Mashirika ya kiraia yanaelezea wasiwasi wake na kutoa wito kwa mamlaka kuwa macho. Yanabainisha kwamba nchi imeteseka sana na inaona jaribio lolote la mapinduzi halikubaliki.
Uchunguzi wa kimahakama umefunguliwa ili kubaini wahusika wa kile ambacho makao makuu ya jeshi yanakielezea kama vitendo vya uhalifu wa mtandaoni.