Serikali imesema matumizi ya nishati safi nchini yameongezeka kutoka asilimia 6 hadi asilimia 28, na kuahidi kuendelea kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali ili kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 13 ya Mradi wa Nishati Endelevu (EnDev) unaotekelezwa na SNV Tanzania, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, amesema mradi huo umenufaisha takribani mikoa 21 kwa kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia na umeme wa jua, hatua inayochangia kupunguza umaskini na kulinda mazingira.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)