Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anazidi kuimarisha uungaji mkono wake kwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Uingereza itasambaza uraniamu iliyorutubishwa kwa Ukraine kwa ajili ya mitambo yake ya nyuklia na kuweka vikwazo vipya kwa Urusi, Waziri Mkuu wa Uingereza ametangaza kabla ya kikao cha mkutano wa kilele cha G7 siku ya Jumanne kuhusu mzozo nchini Ukraine.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ikilaani “mashambulizi ya kikatili” ya Urusi nchini Ukraine, London inakusudia “kuongeza juhudi” kwa “kukata rasilimali zinazochochea vita vya Putin na kutoa nishati kwa Ukraine kwa majira ya baridi kali yajayo,” Keir Starmer alisema katika taarifa iliyorushwa Jumatatu jioni.

Zelensky anatarajiwa katika mkutao wa G7

Takriban pauni milioni 210 (euro milioni 243) katika ufadhili wa mauzo ya nje zitawezesha kampuni ya Uingereza ya Urenco kusambaza uraniamu iliyorutubishwa kwa kampuni inayozalisha nishati ya nyuklia ya Ukraine EnergoAtom, Downing Street ilisema katika taarifa. “Tutasimama na Ukraine kwa muda mrefu iwezekanavyo, na tangazo hili linasisitiza hilo,” Waziri Mkuu wa Uingereza alibainisha.

Rais wa Ukraine anatarajiwa leo Jumanne asubuhi katika mkutano wa kilele wa G7 katika mji wa Evian nchini Ufaransa kushiriki katika mkutano wa kazi kuhusu amani na usalama kwa ajili ya Ukraine na Ulaya. Emmanuel Macron anatumai kumshawishi mwenzake wa Marekani, Donald Trump, kuweka shinikizo zaidi kwa Urusi katika mkutano huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *