
Wapiganaji wa Hizbullah wakabiliana na wanajeshi vamizi wa Israel kusini mwa Lebanon
Hizbollah ilisema katika taarifayake siku ya Jumatatu kwamba wapiganaji wake, wakitumia maroketi na ndege zisizo na rubani, walizuia kitengo wa Israel waliokuwa na vifaru viwili vya Merkava wakisonga mbele karibu na mji wa Kfar Tebnit, karibu na mji wa kusini wa Nabatieh.
Katika taarifa iliyofuata baadaye jana, Hizbullah ilisema kuwa jeshi la adui limepanag upya askari wake karibu na eneo la kivuko kwa kupelekea wanajeshi na vifaru vitano vya merkava na magari manne.
Haya yanajiri baada ya ndege isiyo na rubani ya Israel kulilenga gari moja na kumuuwa dereva wake. Mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel ni hujuma ya kwanza tangu kutangazwa makubaliano.
Vyombo vya habari vya lugha ya Kiebrania wakati huo huo viliripoti “tukio kubwa la usalama” kwa wanajeshi wa Israel walioko kusini mwa Lebanon.
Vyombo hivyo viliongeza kuwa helikopta za shughuli za uokoaji za Israel zinajaribu kuwasafirisha hospitali askari majeruhi huko kaskazini mwa ardahi zinazokaliwa kwa mabavu.
Hata hivyo hakuna ripoti iliyotolewa kuhusu idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa au kujeruhiwa.
Vyombo vya habari vya Israel pia viliripoti kuwa mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni alijiuwa Jumapili usiku kusini mwa Lebanon kutokana na msongo wa mawazo.