
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezuru Haiti siku ya Jumanne, Juni 16. Akipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toussaint Louverture na Waziri Mkuu Alix Didier Fils-Aimé na wajumbe kadhaa wa serikali, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alikutana na viongozi, wawakilishi wamashirika ya kiraia, na kufanya ziara kadhaa za kutathmini ukubwa wa mgogoro nchi hiyo inapitia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Port-au-Prince, Peterson Luxama
Akiwa ameshtushwa sana na kile alichokishuhudia, Antonio Guterres alihutubia waandishi wa habari. Kufuatia ziara yake katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao na mazungumzo yake na waathiriwa wa vurugu hizo, alielezea mgogoro ambao haujawahi kutokea.
“Nimeona mgogoro wa kiwango cha ajabu, ambao chanzo chake ni ukosefu wa usalama. Magenge yanaitishia nchi hii.” Familia nzima zimelazimoshwa kuhaama na kualazimika kutoroka makazi yao. Watoto wananyimwa ulinzi, elimu, na mustakabali. Kwa Wahaiti, kila siku ni mapambano ya kuishi,” alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Watoto kuingizwa katika magenge
Ukosefu wa chakula na kulazimishwa kuhama kwa watu, kunakosababishwa na vurugu za magenge, ni majanga mengine yanayozidisha mgogoro huo, kulingana na Antonio Guterres, ambaye pia alizungumzia uandikishaji wa watoto katika makundi yenye silaha. “Sasa, hadi mmoja kati ya wapiganaji wawili katika magenge hayo ni mtoto. Hii ndiyo asili halisi ya makundi haya: yanastawi kwa kuwanyonya walio katika mazingira magumu zaidi. Hili halivumiliki kabisa; lazima likome,” mwanadiplomasia huyo alitangaza.
Kutokana na hali hii ya kutisha, Antonio Guterres alihakikisha kwamba Umoja wa Mataifa hatokubali nchi hii iendelee kuteseka. “Wahaiti hawako peke yao; Umoja wa Mataifa unasimama nao.” “Dunia inapaswa kuwajibika,” alitangaza.
Kama Katibu Mkuu alibainisha tena kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kwa Haiti, raia wengi walioko wanaendelea kuhoji matokeo halisi ya mipango mbalimbali ya kimataifa iliyotekelezwa kwa miaka mingi ili kusaidia nchi hiyo kupata ahueni ya kudumu kutokana na mgogoro huo.