Mahakama nchini Comoro imekataa siku ya Jumanne, Juni 16, 2026, uwezekano wowote wa kusafirishwa kwa ajili ya matibabu kwa rais wa zamani Ahmed Abdallah Sambi, aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela. Afya ya mkuu huyo wa zamani wa nchi imechochea mjadala mkali nchini kwa wiki kadhaa na hata imesababisha kuwekwa kwa waandishi wa habari wawili chini ya usimamizi wa mahakama.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moroni, Abdallah Mzembaba

Nchini Comoro, ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma ilitangaza msimamo wake kuhusu uwezekano wa kusafirishwa kwa rais wa zamani Ahmed Abdallah Sambi kwa ajili ya matibabu katika mkutano na waandishi wa habari uliotarajiwa sana siku ya Jumanne, Juni 16, 2026. Kulingana na Mwanasheria Mkuu Ahamada Hamidou, hakuna sababu ya kusafirishwa haraka nje ya nchi kwa mkuu huyo wa zamani wa nchi kwa ajili ya matibabu. Hakimu huyo hata alisema kwamba angeruhusu hilo kama madaktari wangependekeza hivyo.

Hitimisho lililotolewa na mamlaka haraka lilisababisha hisia kali kutoka kwa umma, hasa kutokana na kutokubaliana kuhusu tafsiri ya vipimo vya kimatibabu vilivyofanywa kwa ombi la ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma.

Ili kuunga mkono msimamo huu, mamlaka ilitegemea maoni ya Dkt. Saïd Moussa, mkuu wa kitengo cha ganzi na wagonjwa mahututi katika Hospitali ya El-Maarouf, ambaye pia alikuwepo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Mwanasheria Mkuu. Kulingana naye, maisha ya mgonjwa hayako hatarini hata kidogo, na hakuna vigezo vya kimatibabu vinavyohalalisha, katika hatua hii, rais huyo wa zamani kusafirishwa nje ya nchi.

Hata hivyo, daktari alibainisha kwamba hajamfanyia vipimo Ahmed Abdallah Sambi, yeye kibinafsi. Tathmini yake inategemea uchambuzi wa faili ya kimatibabu na mazungumzo yake na timu ya madaktari watano walioteuliwa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu ili kuchunguza afya ya rais huyo wa zamani.

Mamlaka inatatafuta maoni ya daktari wa kigeni

Timu hii ilihitimisha kuwa mkuu huyo wa zamani wa nchi yuko katika hatari kubwa ya moyo na mishipa na inapendekeza angiografia ya moyo, vipimo ambvyao hvipatikani kwa sasa nchini Comoro. Dkt. Saïd Moussa, kwa upande wake, alikiri kutokubaliana na waandishi wa ripoti hii, lakini alibainisha kwamba uchunguzi mbadala unaweza kufanywa ndani ya nchi kabla ya kuzingatia chaguzi zingine.

Kutokana na tafsiri hizi tofauti, mamlaka ilitangaza nia yake ya kutafuta maoni ya daktari wa kigeni au kampuni ili, kulingana na wale waliohusika, kuondoa tuhuma zozote za kuingiliwa na kuendelea na tathmini ya faili ya matibabu ya rais wa zamani, bila, hata hivyo, kutaja tarehe ya kuwasili kwa daktari huyo wa kigeni.

Binti wa Rais wa zamani Ahmed Abdallah Sambi, Wakili Tisslame Sambi, alijibu, akisema alikasirika baada ya uamuzi wa Mwanasheria Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *