VIWANJANI: “Hakuna kipigo kikubwa ambacho kimetokea licha ya kuwa kuna ongezeko la timu nyingi ambazo ni mara ya kwanza zinashiriki.”
Mchambuzi wa soka, @michaelhyera_ amesema mzunguko wa kwanza wa makundi wa Kombe la Dunia 2026 umeonesha ushindani mkubwa, huku timu nyingi zinazoshiriki kwa mara ya kwanza zikionesha kiwango bora.
Hyera amesema tofauti na matarajio ya wengi, timu hizo zimeingia kwenye mashindano kwa maandalizi imara na kuweza kushindana kwa ujasiri dhidi ya mataifa yenye historia kubwa katika soka la dunia.
#Viwanjani
(Feed generated with FetchRSS)