- Shiru Stuart alimkosoa mume wa marehemu Betty Bayo, Tash, kuhusu mapato ya kazi za ushawishi ya binti yake, Sky Victor
- Sky Victor alimtetea babake wa kambo, akimtaka Shiru kuacha kuibua drama za kifamilia na badala yake ajikite katika utengenezaji wa maudhui
- Msichana huyo wa umri wa ujana pia alidai kuwa marafiki wa mamake walimtelekeza yeye na familia yao baada ya kifo chake mwaka 2025 na hawajawahi hata kuwatembelea
Shiru Stuart amemjibu binti wa rafiki yake wa karibu aliyefariki, Betty Bayo, baada ya Sky kumkosoa vikali.

Source: UGC
Betty Bayo alifariki kutokana na saratani mnamo Novemba 2025 na akazikwa tarehe 20 Novemba 2025 katika ardhi yake iliyoko Mugumo Estate, Kaunti ya Kiambu.
Shiru alikuwa ameshiriki ujumbe uliodokeza kuwa mume wa Betty Bayo, Hiram Gitau maarufu kama Tash, alikuwa akichukua fedha ambazo binti yake, Sky Victor, hupata kupitia kazi za ushawishi wa bidhaa na huduma.
Je, Tash anachukua fedha za Sky Victor kutoka kwa kampuni zinazomtumia kufanya matangazo?
Ujumbe wa mafumbo wa Shiru haukumfurahisha Sky, ambaye alijitokeza kumtetea babake wa kambo, Tash.
Wakati wa TikTok Live, Sky alimkemea shangazi yake huyo, akimtaka akae mbali na familia yao.
Alisema matamshi ya Shiru yalikuwa yanamuumiza yeye na familia yake, akimshauri aendelee tu na kazi yake ya kuunda maudhui.
“Acha, acha, acha. Hata kama unaenda kila mahali ukisema unatulinda, unafanya madhara zaidi, unatugawa na kuleta drama zisizo za lazima. Hii inatuumiza zaidi kuliko kutusaidia. Kwa hivyo acha kusema unayosema. Endelea kuchapisha maudhui yako ya kawaida… acha kutusaidia. Unaniumiza kwa kusema mambo hayo yote. Inauma mtu anaposema mambo mabaya kuhusu baba yako…” alisema Sky.
Sky pia alidai kuwa marafiki wa mamake waliwatelekeza baada ya kifo chake mwezi Novemba 2025, baada ya watumiaji wa TikTok kutaja majina ya baadhi ya watu maarufu kwenye sehemu ya maoni.
“Hakuna hata mtu mmoja anayetuangalia. Hawaji nyumbani kwetu. Baada ya mama yetu kufariki, nao walituacha. Hakuna anayetuangalia. Kama unajua ulikuwa rafiki wa mama yetu na hujawahi kuja nyumbani kwetu…” alisema Sky huku akionekana mwenye hisia kali.
Mama huyo wa watoto wawili anayeishi Uingereza alimjibu msichana huyo wa ujana, akiapa kutowahi tena kumtetea au kumsemea Sky.
Shiru, ambaye aliwahi kuwakaribisha Sky na Danny nchini Uingereza baada ya kifo cha mamake mwaka 2025, alikiri kuwa alishtushwa na jinsi Sky alivyoitikia ujumbe wake.
“Nimejionea mwenyewe na nimesikia pia kwamba kila kitu nilichosema kilikuwa uongo. Pia niliambiwa nimwache baba yao. Sawa tu. Tuendelee na maisha! Nilisikia sehemu ya mawaidha yangu. Lakini nilichosikia leo kimenishtua kabisa,” alisema.

Source: Facebook
Kwa nini binti wa Betty Bayo, Sky, alimfukuza kazi yaya wao?
Katika habari nyingine, watoto wa Betty Bayo, Danny na Sky Victor, walieleza sababu zilizowafanya wamfukuze kazi yaya wao katika mazingira yaliyokuwa ya kusikitisha.
Wakati wa TikTok Live, ndugu hao walisimulia mazingira magumu waliyoishi baada ya kifo cha mamake, wakifichua jinsi tabia kali ya yaya huyo ilivyowaathiri kihisia katika kipindi ambacho tayari kilikuwa kigumu kwao.
Sky alidai kuwa yaya huyo alikuwa mkali na alimnyanyasa baada ya kifo cha mamake, madai ambayo Danny pia aliyathibitisha.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke


