Wakikutana Ghana kuanzia Juni 17 hadi 19 kwa ajili ya mkutano mkuu wa kwanza ulioandaliwa tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria la Umoja wa Mataifa kuhusu athari ya utumwa mnamo mwezi Machi mwaka huu, viongozi wa Afrika na wawakilishi kutoka Karibiani wanajaribu kubadilisha hatua hii ya kidiplomasia ya kiishara kuwa mapendekezo halisi.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu maalum huko Accra,

Hata kabla ya kuingia kwenye kumbi za mkutano, wakuu wa nchi waliohudhuria mkutano huko Accra walikaribishwa na malango mawili makubwa yanayoitwa “Doors of Return” [“Milango ya Kurudi”, kwa Kiswahili] yaliyowekwa kwenye mlango wa Hoteli ya Kempinski. Historia inasimuliwa kinyume wakati huu: ambapo “Milango ya Kutorudi” iliashiria kuondoka kwa nguvu utumwani, malango haya yanamanisha kurudi kwa ishara barani Afrika.

Mpango huu unajumuisha azma ya mkutano huu kuhusu malipo ya fidia yanayohusiana na utumwa na ukoloni. Kwa siku tatu, wakuu wa nchi za Kiafrika, viongozi wa Karibiani, na wawakilishi wa raia wa Afrika waihio nje ya bara hilo wanajaribu kufafanua msimamo wa pamoja kufuatia kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwaka jana kuhusu athari ya biashara ya utumwa ya kuvuka Atlantiki.

“Kurejesha heshima”

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, Rais wa Liberia Joseph Boakai, Rais wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah, na Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley.

Kwa Bassirou Diomaye Faye, suala la fidia linazidi kiwango cha kifedha pekee. Ni sehemu ya juhudi pana zinazolenga “kurejesha heshima” ya watu wa Afrika. Rais wa Ghana John Mahama, aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika (AU) kuongoza mpango huu, alisisitiza jukumu kuu la diaspora katika mchakato huu. “Wazao wa wale walioteseka kwa utumwa sio waangalizi tu wa mchakato huu. Wao ndio walioathiriwa moja kwa moja,” alisema.

Kutoka kumbukumbu hadi mifumo halisi

Zaidi ya matamko ya kanuni, washiriki kadhaa pia walisisitiza hitaji la kufafanua mifumo halisi. Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley aliwasilisha mpango wa pointi kumi wa Jumuiya ya Caribbean (CARICOM), ambao unajumuisha hatua zinazohusiana na maendeleo, uhamisho wa teknolojia, na unafuu wa madeni.

Kwake, athari ya utumwa haizuiliwi na kupoteza wafanyakazi tu. “Kilichochukuliwa kutoka Afrika kuvuka Atlantiki haikuwa nguvu kazi tu, bali pia mawazo, ubinadamu, sanaa, na utamaduni,” alisema.

Katika ujumbe wa video kwa washiriki, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alibinisha kwamba Ufaransa iliunga mkono kikamilifu mpango unaoongozwa na Ghana, licha ya Paris kutofanya hivyo wakati wa kupiga kura kuhusu azimio la Umoja wa Mataifa.

John Mahama alitangaza zaidi kuundwa kwa majopo matatu ya kimataifa yaliyojitolea kwa haki ya kurejesha, urejeshaji wa mali ya kitamaduni, na njia za kisheria za kuendeleza suala hili.

Washiriki wanatarajiwa kupitisha tamko la mwisho mwishoni mwa mkutano huo, kwa lengo la kubadilisha kasi inayotokana na azimio la Umoja wa Mataifa kuwa mpango wa utekelezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *