Hivi ndivyo Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Kenan Kihongosi alivyopokelewa kwa shangwe na furaha na wakazi wa Iringa mjini hapo jana alipowasili kwa ziara maalum ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kukagua uiamara wa Chama lakini pia kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Iringa mjini mkoani Iringa.
Mapokezi hayo yaliyonogeshwa na kupambwa na vijana maafisa usafirishaji wa bodaboda Pamoja na Bajaji wa Iringa mjini kwa Kiongozi huyo wa Chama Tawala CCM yameonesha ishara ya mapenzi makubwa na imani ya wakazi wa mkoa huo kwa Chama cha Mapinduzi lakini kwa Serikali inayoongozwa na Chama hicho chini ya Mwenyekiti wake ambae ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kenan Kihongosi kama apendavyo kujiita ‘Mtumishi wa wote’ alionyesha kwa vitendo kauli yake hiyo pale alijishusha na kuamua kuungana na vijana hao kwa kupanda bodaboda akiwa ameongozana nao
kuelekea katika uwanja wa Mwembetogwa
ulikofanyika mkutano wa hadhara hapo Iringa Mjini.
Katika Mkutano huo Katibu Mwenezi huyo alipata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa Wilaya hiyo na kusikiliza kero zao mbalimbali ambapo baadhi alizitafutia ufumbuzi wa papo kwa hapo huku zingine akiahidi kuzifikisha Serikalini kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Kenan Kihongosi amehitimisha ziara yake ya siku tatu katika mkoa huo baada ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali, kuangazia uimara wa chama na kusikiliza kero za wananchi katika maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Kilolo pamoja na Iringa mjini ikiwa ni mkoa wa 13 tangu aanze ziara zake.
(Feed generated with FetchRSS)