Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Ndugu Kenani Laban Kihongosi, ameweka wazi baadhi ya kauli za zamani za Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa mwanachama na mmoja wa viongozi wa Chama cha Upinzani cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambae mwaka juzi 2024 alitangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama Tawala cha Mapinduzi CCM na mwaka huu tena akatangaza kuhama CCM na kurudi katika chama chake cha zamani cha CHADEMA ambapo ameeleza kuwa kitendo hicho cha kutokuwa na msimamo unaoeleweka ni ushahidi unaoonesha mabadiliko ya misimamo yenye lengo la kuwapotosha wananchi kwa manufaa ya kisiasa.

Kihongosi ameyasema katika mkutano wa hadhara uliofanyika Iringa mjini hapo jana wakati wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo.

Aidha Kihongosi amesema viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa waaminifu kwa wananchi na kusimamia wanachokiamini wakati wote, badala ya kubadili misimamo kulingana na mazingira ya kisiasa.

Mchungaji Peter Msigwa ambae alikuwa mbunge wa zamani wa CHADEMA Jimbo la Iringa Mjini na ambae pia amewahi kushika nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho kanda ya Nyasa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alitangaza uamuzi wake wa kukihama chama hicho cha CHADEMA mnamo mwezi June 2024 na kuhamia CCM

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *