Kwa miaka minane iliyopita, mamlaka ya Ubelgiji na Kongo zimekuwa yakifanya kazi kwa bidii katika kurejesha vitu vya sanaa na urithi vilivyochukuliwa na mara nyingi kuporwa wakati wa ukoloni wa kile kilichokuwa Kongo Huru na baadaye Kongo ya Kibelgiji.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Bénazet

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Judith Suminwa Tuluka, amemwandikia mwenzake wa Ubelgiji, Bart De Wever, kuomba rasmi kurejeshwa kwa mamia ya mafuvu ambayo “yalikusanywa” wakati wa ukoloni.

Mbali na makusanyo ya Jumba la Makumbusho la Kifalme la Afrika ya Kati huko Tervuren, ambayo yanafanya orodha ndefu kwa ajili yakurejesha mabaki mbalimbali katika jumba la makumbusho huko Kinshasa, pia kuna “makusanyo”  ya vitu vya kijamii, kitamaduni, na kisayansi yanayotiliwa shaka kubwa, yaani mafuvu ya Waafrika yaliyohifadhiwa katika makumbusho ya Ubelgiji.

Mabaki zaidi ya 500 ya binadamu, hasa Wakongo lakini pia Wanyarwanda na Warundi, yanaaminika bado yanahifadhiwa katika taasisi za Ubelgiji.

Kwa muongo mmoja uliopita, mamlaka ya Ubelgiji imekuwa ikitathmini upya urithi wa ukoloni wa nchi yao. Kulingana na serikali ya shirikisho, mabaki ya binadamu yaliyoletwa Ulaya kama nyara au vitu vya kitamaduni katika karne ya 19 na 20 hayana nafasi katika makumbusho mwaka wa 2026.

Wanasayansi kutoka kikundikazi kilichoteuliwa na Bunge la Ubelgiji wameamua kwamba “mabaki yote ya kihistoria ya binadamu yanayohusiana moja kwa moja na historia ya ukoloni ya Ubelgiji” lazima yarudishwe.

Waziri Mkuu wa Kongo anasisitiza katika barua yake kwamba sampuli zilizohifadhiwa katika Jumba la Makumbusho la Sayansi Asilia huko Brussels ni za wafu ambao “lazima waweze kupumzika kwa heshima katika nchi yao ya asili na hawawezi kuchukuliwa kama vitu vya urithi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *