Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MH. DK. SAMIA SULUH HASSAN amewaagiza wataalamu wa tafiti za magonjwa ya saratani nchini kushirikiana na wataalamu wengine kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu za ongezeko la visa vya saratani na magonjwa kwa watoto ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa mapema kudhibiti tatizo hilo.
Akizungumza baada ya kuzindua jengo la tiba ya mionzi Dk. SAMIA SULUH HASSAN anaagiza kufanyika kwa utafiti huo ili kubaini chanzo cha magonjwa ya saratani na moyo kwa watoto wadogo.
Waziri wa afya MOHAMMED MCHENGERWA amesema uzinduzi wa jengo hilo ni ishara ya mafaniukio ya serikali katika kusogeza karibu huduma kwa wananchi.
Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya kanda ya KCMC Askof ALEX MALASUSA anamuomba Mh. Rais kutoa msamaha wa kodi utakasaidia uagizwaji wa vifaa tiba katika taasisi ya moyo pamoja na jengo la tiba ya mionzi ili kuboresha huduma za matibabu hayo.
(Feed generated with FetchRSS)