
Seneti ya Marekani imepiga kura ya kuidhinisha azimio la kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kwenye vita na Iran, katika hatua ambayo imetajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni kielelezo cha pigo la kisiasa kwa Rais Donald Trump.
Azimio hilo limepitishwa kwa wingi wa kura 50 dhidi ya 48, lakini kutokana na sheria za kongesi, rais hatahitaji hata kutumia kura yake ya turufu dhidi yake. Hata hivyo, kura hii ni pigo kwa Trump katika kipindi hiki ambapo Marekani iko katikati ya mazungumzo na Iran, huku chama chake kikiwa na wingi katika Baraza la Wawakilishi na Seneti.
Azimio hilo linamtaka Rais wa nchi kuomba idhini Kongresi kabla ya kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran.
Kura hii ya Seneti ya Marekani inafuatia idhini ya Baraza la Wawakilishi kwa hatua hiyo hiyo mapema mwezi huu.
Ingawa azimio hilo halina nguvu ya kiutekelezaji na halihitaji sahihi ya rais, lakini kupitishwa kwake kunawakilisha msimamo rasmi wa upinzani wa mabunge mawili ya Marekani dhidi ya uchokozi wa nchi hiyo nchini Iran.
mnamo Aprili 7, Trump alilazimika kutangaza usitishaji mapigano katika uchokozi wa karibuni wa Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Tangazo hilo lilifuatia angalau raundi 100 za mashambulizi makali ya kulipizia kisasi ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi na maeneo nyeti na ya kimkakati ya Marekani na Israel katika eneo lote la Magharibi mwa Asia.
Wakati huo huo, uchunguzi wa maoni uliofanywa na Reuters/Ipsos umefichua wasiwasi mkubwa wa umma nchini Marekani kuhusu sera ya Rais Donald Trump kuhusu Iran, huku Wamarekani watatu kati ya kila wanne wakipinga vita vya nchi hiyo dhidi ya Iran.