Takriban mashirika 38 yasio ya kiserikali, yakiwemo Amnesty International na Human Rights Watch yametoa wito wa hatua za kimataifa kuchukuliwa kuzuia ukatili kutokea katika mji wa El-Obeid nchini Sudan.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika barua ya wazi kwa wanachama na nchi waangalizi katika baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, mashirika hayo yameitaka baraza hilo kushughulikia kwa haraka hali ndani yam ji wa El-Obeid na maeneo yanayouzungumka mji huo, na kuchukua hatua Madhubuti kuzuia ukatili na kuhakikisha uwajibikaji.

Wito wao unajiri licha ya umoja wa mataifa kuelezea hofu ya kushuhudiwa tena matukio ya Oktoba 2025 katika mji wa El-Fasher wakati wapiganaji wa RSF walipoingia kwenye mji huo.

Wito wa kimataifa umekuwa ukiongezeka kuhusu hali katka mji wa El-Obeid, huku maonyo makali yakitolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi kadhaa za Ulaya katika wiki iliyopita.

Mashirika hayo pia yamezitaka nchi wanachama wa baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa kuzikashifu wahusika wan je wanaounga mkono pande hasimu ikiwemo nchi ya umoja wa falme za kiarabu, ambayo hata hivyo imekanusha kuingilia mzozo wa Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *