Baadhi ya watu wenye ulemavu katika halmashauri ya mji wa mbinga mkoani ruvuma ambao wamenufaika na mkopo wa asilimia 10 unaotokana na mapato ya ndani wametakiwa kuchangamkia fursa ya kuomba mikopo hiyo ili waweze kukuza ujasirimali, ubunifu,, ajira pamoja na kuimarisha kipato na kukuza uchumi na mtu mmoja.

Wito huo umetolewa na Maria Chiwinga ambaye ni mlemavu anayejishugulisha na ukopeshaji wa nguo na vikapu alivyotengeneza baada ya kunuifa na mkopo huo ambapo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu hassan kwa kuidhinisha mikopo hiyo, huku akiwataka wenye ulemavu wasijisikie vibaya kwa kukaa majumbani badala yake amewataka wajiunge katika vikundi ili wapatiwe kwa kuwa inatolewa bila ubaguzi.

Akikabadhi mfano wa hundi ya zaidi ya shilingi milioni 325 kwa vikundi 19 vya wanawake,vijana na watu wenye, mkuu wa wilaya ya Mbinga Kisare Makori amewataka waliopatiwa mikopo hiyo kuwa na mipango mizuri ya biashara ili waweze kurejesha mikopo kwa wakati pqmoja na nidhamu ya fedha katika matumizi.

Kwa upande wa afisa maendeleo ya jamii Halmashauri Cecilia Mbata amesema jumla ya wanufaika 210 wamepatiwa mikopo hiyo katika kata 16 za Halmashauri ya mji wa Mbinga.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *