Mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewaongoza maafisa wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kupanda Miti katika shule ya sekondari Mara sekondari pamoja na hospital ya Rufaa ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Maarufu KWANGWA katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya malaka hiyo toka kuanzishwa Julai mosi mwaka huu.

Akizungumza katika zoezi hilo meneja wa Mamlaka hiyo mkoani Mara Masawa Masatu amesema upandaji wa miti nikurejesha uoto katika maeneo yanayoizunguka jamii hivyo mamlaka hiyo imetekeleza jukum hilo ikiwa nimkakati wa kuweka alama katikamkutimiza miaka 30 ya mamlaka hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewataka wenyevti wa mitaa na watendaji kuhakikisha wanasimamia uwekaji wa mazingira sawa katika maeneo yao ikiwemo kupanda miti kama ilivyolekezwa na zoezi hilo litafanyika kila kaya.

“Zoezi hili linapaswa kuwa nilasiku zote tunahitaji kuona mti kwa kila kaya tutakapopita hata nikwenye taasisi hilo litekelezwe na kila mtu nanyie viongozi lisimamieni”Alisema Mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *