n

Chanzo cha picha, caf

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 4

Ingawa bara la Afrika limezalisha baadhi ya wachezaji bora na wenye vipaji, lakini vyama vya soka katika mataifa mengi, vimekuwa vikitafuta makocha kutoka nje.

Mafanikio ya timu za Afrika, yaliongozwa na tamaduni ya kuajiri wazungu kutoka Ulaya au Amerika Kusini wenye uzoefu na utaalamu ili kuongoza timu za Afrika kwenye michezo ya kimataifa kama Kombe la Dunia.

Hata hivyo, mabadiliko makubwa yanatokea katika soka la Afrika. Makocha ambao ni wazawa wa Afrika wameanza kuchukua nafasi kubwa. Makocha ambao wanaelewa utamaduni, saikolojia, na vinasaba vya soka la Afrika.

Kombe la Dunia la FIFA la 2026 linaloendelea linaonyesha mapinduzi haya waziwazi, kukiwa na makocha kadhaa waliozaliwa Afrika au wa asili ya mataifa ya Afrika. Wakionesha uzoefu wao kimataifa, mbinu na uelewa wa soka.

Pape Thiaw – Senegal

m

Chanzo cha picha, CAF

Baada ya kuondoka kocha wa muda mrefu Aliou Cissé, Senegal haikuenda Ulaya kumsaka mrithi wake. Badala yake, walimwamini Pape Thiaw, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa ambaye alicheza pamoja na Cissé wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia ya 2002.

Akiwa tayari ameifundisha timu ya Senegal kwenye michuano ya CHAN, Thiaw alijitosa bila shida kuongoza timu ya wakubwa kupitia kampeni yenye mafanikio na kufuzu kwenda Kombe la Dunia.

Falsafa yake ya kimbinu inachanganya muundo wa ulinzi na mabadiliko ya haraka ya kushambulia, tayari amepata ushindi mkubwa wa 5-1 katika hatua ya makundi dhidi ya Iraq kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.

Emerse Faé – Côte d’Ivoire

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Emerse Faé akiwa meneja wa muda katikati ya kiwango kibaya wakati wa AFCON ya 2023 nyumbani, Faé aliifufua timu ya Ivory Coast iliyokuwa imekufa.

Alileta imani ya kisaikolojia, marekebisho ya kimbinu, na uongozi, akiwaongoza Elephants kwenye taji la bara. Baada ya kupewa mkataba wa kudumu, Faé alifanikiwa kuibadilisha timu hiyo na kuipeleka kwenye jukwaa la kimataifa.

Mbinu zake katika uchezeshaji hutegeme nguvu ya kiungo, kasi ya wachezaji wa winga, bila shaka na mawaidha katika chumba cha kubadilishia nguo.

Pedro “Bubista” Brito – Cape Verde

,l

Chanzo cha picha, gety images

Pedro Leitão Brito, anayejulikana kama Bubista, amebuni mojawapo ya hadithi za kuvutia kwa timu ambayo inacheza kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia.

Akiiongoza taifa dogo la kisiwa cha Cape Verde tangu 2020, nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ameongoza timu kwa utulivu, mpangilio, na mwendelezo wa kimbinu.

Mafanikio ya Bubista yalikuja kwa kuwaongoza Blue Sharks kwenye mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia, ambapo wamewashangaza mashabiki duniani kote kwa kupata sare ya 0-0 dhidi ya Spain, Saudi Arabia, na sare ya 2:2 dhidi ya Uruguay, na kuwafanya kusonga mbele.

Mohamed Ouahbi – Morocco

mm

Chanzo cha picha, Getty Images

Kachukua mikoba baada ya mbio za kihistoria za nusu fainali za Walid Regragui mwaka 2022, Mohamed Ouahbi mzaliwa wa Morocco ameichukua nafasi hiyo kwa ujasiri wa hali ya juu.

Akipandishwa cheo kutoka timu ya taifa ya vijana miezi michache tu kabla ya mashindano, Ouahbi anakitumia vyema kizazi kipya cha vipaji cha Morocco.

Anaendeleza mpangilio mzuri wa ulinzi wa Regragui huku akianzisha mtindo wa kiufundi unaozingatia umiliki wa mpira ambao umewapeleka Atlas Lions katika Raundi ya 32.

Sabri Lamouchi – Tunisia

m

Chanzo cha picha, Le

Ni raia wa Tunisia na Ufaransa, aliyezaliwa Ufaransa na wazazi wa Tunisia, Sabri Lamouchi ana ya mafanikio akiwa kiungo wa kati barani Ulaya na safari yake ya ukocha katika ngazi za vilabu na timu za taifa.

Lamouchi alianzia soka lake la kulipwa nchini Ufaransa katika klabu ya Olympique Alès kabla ya kufanikiwa zaidi akiwa na AJ Auxerre, ambako alishinda mataji mawili makubwa: Ligue 1 na Coupe de France mwaka 1996.

Kwa nini makocha wazawa?

Mafanikio yanayoonekana ya mameneja hawa yameondoa kabisa dhana potofu kwamba mbinu za makocha wa kigeni ni bora zaidi. Mafanikio ambayo makocha wa Afrika huleta kwa timu ya taifa ya Afrika ni kubwa.

Kocha kutoka Afrika anaelewa tofauti za kijamii, lugha, na changamoto wanazokabiliana nazo wachezaji wao. Wanajua jinsi ya kuwaunganisha wachezaji waliozaliwa ugenini na wale waliolelewa katika ligi za ndani.

Kwa makocha wa ndani, kazi ya ukocha sio kazi ya malipo tu au ujenzi wa wasifu wake. Ni kitendo cha huduma kwa kitaifa. Muunganisho wa kihisia kati yao na wachezaji ni muhimu katika mafanikio.

Kwa kuongozwa na mafanikio makubwa ya makocha hawa, jumuiya ya mpira wa miguu duniani haiwaoni tena mameneja wa Kiafrika kama kitu kipya. Wanaonekana kama wataalamu bora ambao wamejipatia nafasi zao, wakiongoza mataifa yao kuelekea ndoto ya kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *