Chama cha Waagizaji Mafuta Tanzania (TAOMAC) kimesema Tozo ya Maendeleo ya Miundombinu ya Bandari (PID Levy) ni uwekezaji wa kimkakati utakaoongeza ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam, kupanua uwezo wake wa kupokea meli kubwa za mafuta, kuongeza biashara ya nishati kwa nchi za Zambia, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuimarisha mnyororo wa thamani wa biashara hiyo na hatimaye kuwanufaisha wafanyabiashara, walaji na uchumi wa Taifa kwa kupunguza gharama za uagizaji na usafirishaji wa mafuta kwa muda mrefu.
Akizungumza kuhusu umuhimu wa PID Levy, Mkurugenzi Mtendaji wa TAOMAC, Raphael Mgaya, amesema ingawa baadhi ya watu wanaweza kuitazama tozo hiyo kama gharama ya ziada kwa sasa, ukweli ni kwamba manufaa yake yataonekana kadri uwekezaji wa miundombinu ya bandari utakavyoongeza ufanisi wa huduma na kuvutia shehena nyingi zaidi kupita nchini.
Mgaya amesema Bandari ya Dar es Salaam tayari ni kitovu muhimu cha biashara ya mafuta kwa nchi kadhaa zisizo na bandari, hivyo kuendelea kuwekeza katika miundombinu yake kutaiwezesha Tanzania kuimarisha nafasi yake kama lango kuu la biashara ya nishati katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)