Bamako – Baraza kuu la mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) imeeleza kusikitishwa kwake na hatua ya mataifa ya Mali, Burkina Faso na Niger kujiondoa kwenye mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kamati hiyo imesema kujiondoa kwa mataifa hayo kwenye mahakama hiyo kunadhoofisha juhudi zinazoendelea za kutafuta haki duniani.

Kupitia taarifa, kamati hiyo inayojumuisha mataifa wanachama yaliyounda mkataba wa Roma imeongeza kuwa imesikitishwa na nchi hizo tatu kujiondoa kama wanachama.

Mali, Burkina Faso na Niger walitangaza mpango wa kujiondoa mwaka uliopita kwa misingi kuwa mahakama ya ICC imekuwa ikitumika kama chombo cha kinaendeleza ukolobi mambo leo miongoni mwa mataifa ya Africa.

Mahakama ya ICC ina mataifa wanachama 125, ila baadhi ya mataifa yenye ushawishi duniani kama vile China, India, Israel, Urusi na Marekani zilikataa kujiunga kuwa wanachama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *