Rais wa Msumbiji kuwasili leo DarRais wa Msumbiji kuwasili leo Dar

DAR ES SALAAM:Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Francisco Chapo, anatarajiwa kuwasili nchini leo jioni kwa ziara ya kikazi. Akiwa nchini, Rais Chapo atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Chapo atakuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), utakao fanyika Julai 3, 2026, katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo inalenga kuendeleza uhusiano wa kidugu na kihistoria, ujirani mwema na ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *