
Mji mkuu wa Ukraine umelengwa na makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi zilizosababisha moto na kuwaua watu wasiopungua wanane siku ya Alhamisi, Julai 2, baada ya Volodymyr Zelensky kuonya kuhusu shambulio “kubwa”. Rais wa Ukraine alibaini siku iliyopita kutoka Dublin kwamba anarudi mara moja Kyiv kufuatia ripoti za shambulio jipya la Urusi lililokuwa likiandaliwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mfululizo wa mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya Kyiv yamesababisha vifo vya watu wasiopungua wanane na “idadi kubwa” ya watu waliojeruhiwa, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji mkuu wa Ukraine, Timur Tkachenko, ametangaza siku ya Alhamisi asubuhi. “Wakati wa usiku, adui alianzisha tena shambulio kubwa dhidi ya jimbo la Kyiv kwa kutumia ndege zisizo na rubani za mashambulizi, makombora ya balistiki, na makombora ya cruz,” Mykola Kalashnyk, mkuu wa utawala wa kijeshi wa jimbo la Kyiv, amesema mapema Alhamisi kwenye Telegram, akibainisha kuwa wilaya tano zimeshambuliwa.
Waandishi wa habari wa AFP walisikia milipuko wakati wa mfululizo wa mashambulizi kwa saa kadhaa. Wingu la moshi lilipanda baada ya mlipuko katikati ya mji mkuu wa Ukraine, likifuatiwa na miale ya moto na makaa ya moto, kulingana na mwandishi wa habari huko Kyiv. Kikosi cha wa zima moto na magari ya wagonjwa walifika haraka katika eneo la tukio. Takriban dakika hamsini baada ya mlipuko wa kwanza, walisikia mlipuko wa pili karibu na eneo la awali la ajali, ambao ulirusha vifusi hewani.
“Katika hatua hii, idadi ya vifo kutokana na shambulio la Urusi imeongezeka hadi wanane. Kwa mara nyingine tena, adui analenga maeneo ya makazi kwa makusudi na kuwaua raia,” ameandika Timur Tkachenko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kyiv, kwenye Telegram, huku mamlaka katikaeneo hilo zikiripoti majengo ya makazi yaliyoharibiwa sana. Alibainisha kuwa maeneo 28 yameathiriwa na mashambulizi hayo, “hasa majengo ya makazi na miundombinu ya raia.”