Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imesitisha shughuli zake kwa muda huko Haut-Mbomou, kusini mashariki mwa nchi. Sababu: hali mbaya ya usalama inayosababishwa na vurugu na mashambulizi yanayowalenga wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Bangui, Rolf Steve Domia-Leu

Upatikanaji wa kibinadamu unazidi kuwa mgumu katika sehemu hii ya kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), haswa huko Zémio, Mboki, na Dembia, ambapo ukosefu wa usalama unavuruga shughuli za timu za misaada na uwasilishaji wa vifaa muhimu. Hali hii inapunguza kwa kiasi kikubwa usaidizi kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi na kuzua wasiwasi mkubwa kuhusu upatikanaji wao wa misaada.

Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), matukio hayo yanapunguza kasi ya shughuli na kuathiri upatikanaji wa jamii zilizonyimwa huduma za msingi, miundombinu, na msaada.

“Kuchukua muda wa kuomba pande zote katika mzozo”

Alban Joseph M’Boligassihe, afisa wa masuala ya kibinadamu wa OCHA, anabainisha: “Kwa sasa tuna wakimbizi wapatao 6,000 huko Haut-Mbomou na takriban wakimbizi wa ndani 20,000.” Ikiwa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu wanashambuliwa, ikiwa kuna visa vingi vya mauaji na vitisho, wakati fulani ni muhimu kuchukua muda wa kuomba pande zote katika mzozo ili kutekeleza shughuli za kibinadamu kwa ufanisi.

Athari za kusiishwa kwa muda kwa shughuli za kiinadamu, hali ya maelfu ya watu ambao tayari wako katika mazingira magumu inaendelea kuzorota, kama Alban Joseph M’Boligassihe anavyoeleza: “Hakuna uhuru wa kutembea. Watu hawawezi kwenda kwenye mashamba yao. Watu wamekwamaa msituni. Ni hali ngumu sana kuvumilia.”

OCHA inatoa wito kwa makundi yenye silaha na pande zinazohusika katika mzozo huo kusitisha uhasama. Hatua hii ni muhimu ili kuruhusu wafanyakazi wa mashirika ya kutoa msaada wa kibinadamu kuendelea na shughuli zao katika maeneo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *