Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu umeendelea kuleta matokeo chanya kwa wananchi, huku ujenzi wa Shule ya Kutwa ya Nyangao Sekondari ukiondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu.
Wakazi wa eneo hilo wamekiambia chombo hiki cha habari kuwa kwa miaka mingi watoto walikabiliwa na njaa, safari ndefu, wanyama hatari na changamoto nyingine walipokuwa wakifuata shule za mbali, lakini sasa huduma ya elimu imewasogelea karibu na makazi yao.
Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Mkuu wa Shule ya Kutwa ya Nyangao Sekondari, Mwalimu Mgeta Mkoi, amesema serikali ilitoa zaidi ya shilingi milioni 560 kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo ya kisasa, ambayo tayari imesajiliwa na kuanza kupokea wanafunzi.
#kilichoborakabisa
(Feed generated with FetchRSS)