Nchini Mali, kufuatia mashambulizi yaliyoratibiwa katika miji kadhaa siku ya Jumamosi, Julai 4, mapigano yameanza tena Jumapili, Julai 5, katika mji wa kaskazini wa Anéfis kati ya jeshi la Mali—linaloungwa mkono na mamluki wa Urusi—na muungano wa wanajihadi unaohusishwa na Al Qaeda na waasi wa Azawad Liberation Front (ALF). Mfululizo wa mashambulizi ya kuvizia na makabiliano makali viliripotiwa siku ya Jumapili.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Siku ya Jumapili hii, Julai 5, waasi walikuwa bado wakidhibiti mji wa Anéfis, eneo la kimkakati kaskazini mwa mbali, na bado walikuwa wakiwashikilia wanajeshi kadhaa wa serikali.

Wakati huo huo, wanajeshi wa serikali na washirika wao wa Urusi kutoka Africa Corps walikimbilia katika kambi ya kijeshi katika eneo hili la kimkakati. Kulingana na taarifa zetu, helikopta za jeshi, ambazo zilikuwa zimekuja kuwaokoa waliojeruhiwa katika kambi ya kijeshi na pengine kuwaletea silaha, hazikuweza kutua na zilishambuliwa mapema mchana.

Milio ya risasi bado ilikuwa ikisikika huko Anéfis mchana wa Jumapili. Chanzo ndani ya jeshi la kawaida kilituambia kwamba “kila kitu kinafanywa kudhibiti haliya mambo.” Waasi, kwa upande wao, wanabainisha kwamba lengo lao ni lile lile: “kuchukua udhibiti wa eneo hilo na kuwaondoa utawala wa kijeshi madarakani.”

Waasi watekeleza shambulio la kuvizia

Kinachoshuhudiwa ni vita vya kudhibiti mji wa kimkakati wa Anéfis, ambavyo vinatarajiwa kuendelea siku ya Jumatatu. Mji huu uko takriban kilomita 100 kutoka mji wa Kidal, ngome ya waasi. Kuchukuwa udhibiti wa Anéfis kutamarisha ngome zao. Hata hivyo, kwa jeshi la Serikali na mamluki wa Urusi, kudumisha udhibiti wa mji huu kutawadhoofisha waasi.

Lakini mapigano mengine ya ardhini yalitokea kusini kidogo, yapata kilomita 140 kutoka mji wa Gao. Waasi walivamia kikosi cha wanajeshi wa serikali waliokuwa wakijaribu kufika Anéfis siku ya Jumapili. Mapigano makali yalitokea, magari yalichomwa moto, helikopta iliharibiwa… msafara, au angalau kile kilichobaki kwa msafara wa jeshi la Mali, ulilazimika kurudi nyuma na wengi waliojeruhiwa.

Mvutano karibu na Gao

Huko Gao, jiji kuu kaskazini mwa Mali, wakazi waliamshwa na milipuko siku ya Jumapili. Mabaki ya ndege isiyo na rubani yalipatikana muda mfupi baadaye kwenye shamba moja. Inaripotiwa kuwa mtu mmoja alijeruhiwa. Hakuna kundi lililodai kuhusika. Hata hivyo, mvutano karibu na jiji unaonekana, kulingana na mashahidi.

Katikati na kusini mwa Mali, hakukuwa na mapigano siku ya Jumapili, kulingana na vyanzo vyetu. Hata hivyo, huko Bamako, mji mkuu, mashahidi waliona msafara wa vifaa vya kijeshi ukiwasili usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, huenda ukitoka nchi jirani.

Serikali ya Mali bado haijatoa majibu kuhusu matukio ya Jumapili. Hii inashangaza kidogo, kwa sababu asubuhi ya Jumamosi, kulikuwa na angalau taarifa mbili rasmi za ushindi, na ukimya wa utawala wa kijeshi siku ya Jumapili umepokelewa na maoni tofauti huko Bamako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *