-Ni la kuboresha ufugaji na tasnia ya maziwa
Dar es Salaam – Mshindi wa kwanza wa Vijana Uchumi Challenge 2026, Geoffrey Samuel Sanga kutoka Dodoma, ameibuka na Sh milioni 50 kutokana na wazo lake la kuboresha sekta ya ufugaji na tasnia ya maziwa nchini.
Akizungumza katika mahijiano na Star TV na Radio Free Africa (RFA) mara baada ya kutangazwa mshindi katika fainali za shindano hilo zilizofanyika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Sanga amesema wazo lake linahusu kuanzishwa kwa National Embryo Transfer Laboratories ili kuboresha mbegu bora za mifugo na kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.
Ameongeza pia wazo hilo linahusisha JOSTASA Farming Hubs zitakazojikita katika uzalishaji, mafunzo, utafiti, teknolojia na masoko kwa lengo la kuimarisha mnyororo wa thamani wa sekta ya mifugo.
Sanga amebainisha kuwa ushindani huo ulipitia hatua ngumu Kati ya. zaidi ya mawazo 7,800 na kupatiana 100 bora na hatikayei 10 bora kabla ya kuibuka mshindi wa kwanza jana mbele ya Waziri Mkuu, Mwigulu aliyemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumzia fedha alizoshinda mshindi huyo amesema zitamwezesha kutekelezaji wa wazo lake, akisisitiza kuwa sekta ya kilimo na mifugo ina nafasi kubwa ya kuanzia na kukua hatua kwa hatua.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliwataka vijana kuendelea kutumia ubunifu wao kuwekeza katika miradi yenye tija badala ya kutegemea ajira pekee.
Shindano hilo limefanyika katika JNICC, Dar es Salaam likiwa na lengo la kuibua na kuendeleza ubunifu wa vijana nchini.
(Feed generated with FetchRSS)