- Moses Wetang’ula ametoa makataa ya saa 48 kwa gazeti la The Standard, akitaka lichapishe kanusho na kuomba radhi kufuatia habari yenye utata
- Spika wa Bunge la Kitaifa anasema ripoti hiyo ilimhusisha kwa uongo na madai ya upendeleo wa kifamilia katika uteuzi wa nafasi za umma
- Kupitia kwa mawakili wake, Wetang’ula ameonya kuwa kushindwa kutimiza matakwa hayo kunaweza kusababisha hatua za kisheria za madai na hata jinai
Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, ametishia kulishtaki gazeti la The Standard kwa kile anachokieleza kuwa ni uchapishaji wa habari za uongo na za kumchafulia jina zilizomhusisha na madai ya upendeleo wa kifamilia katika uteuzi wa nafasi za umma.

Source: UGC
Katika barua ya madai ya tarehe Jumapili, Julai 6, Wetang’ula, kupitia kwa mawakili wake wa Millimo, Muthomi & Co. Advocates, amelipa kampuni hiyo ya habari saa 48 kufuta habari hiyo, kuchapisha ombi la radhi lisilo na masharti na kusitisha usambazaji wowote zaidi wa makala hiyo.

Pia soma
Magazeti ya Kenya, Julai 7: Sifuna kuongoza maporomoko makubwa ODM huku akianza safari kusaka urais
Barua hiyo ilielekezwa kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Standard Group, mhariri mkuu na mwanahabari aliyeandika makala hiyo.
Kwa nini Wetang’ula anatishia kuishtaki The Standard?
Mgogoro huo unatokana na makala ya ukurasa wa mbele iliyochapishwa Julai 6 yenye kichwa cha habari “broad-based family,” iliyomuonyesha Wetang’ula pamoja na watu kadhaa wanaohudumu katika nyadhifa za umma.
Kulingana na spika huyo, uchapishaji huo ulidokeza kwa uongo kuwa watu hao ni ndugu zake ambao walipata nafasi serikalini kupitia ushawishi wake.
Timu yake ya kisheria ilisema makala hiyo ilimwonyesha kama afisa wa umma anayetumia nafasi yake kuwapa ndugu zake uteuzi wenye maslahi makubwa serikalini, jambo linalohusishwa na upendeleo wa kifamilia.
“Uchapishaji huo unaacha bila shaka kwamba mteja wetu ana uhusiano wa kifamilia na watu wote waliotajwa humo na kwamba alitumia uhusiano huo kushawishi uteuzi wao katika nyadhifa za umma. Hivyo basi, uchapishaji huo unamwonyesha mteja wetu, machoni mwa wanajamii wenye fikra timamu, kama mtu anayetumia vibaya ofisi ya umma kuwazawadia ndugu zake nyadhifa za juu serikalini, jambo linalojulikana kama upendeleo wa kifamilia, pamoja na maovu mengine,” mawakili hao walisema.
Wetang’ula ameyataja madai hayo kuwa ya uongo, yenye nia mbaya na ya kumchafulia jina.
Je, ndugu wa Wetang’ula wanashikilia nyadhifa za juu serikalini?
Kulingana na barua hiyo ya madai, ndugu pekee aliyetajwa katika uchapishaji huo ni mdogo wake, Tim Wanyonyi, ambaye ni Mbunge wa eneo la Westlands baada ya kuchaguliwa na wapiga kura.
Mawakili hao walisisitiza kuwa hakuna mtu mwingine yeyote aliyepo kwenye makala hiyo ambaye ana uhusiano wa kifamilia na spika huyo, na kwamba wote wanashikilia nyadhifa zao kwa msingi wa uwezo na sifa zao binafsi, si kutokana na uhusiano wa kifamilia.
“Hakuna yeyote kati ya watu waliotajwa katika uchapishaji wenu ambaye ana uhusiano wa kifamilia na mteja wetu, isipokuwa mdogo wake, Mhe. Tim Wanyonyi. Watu hao wanashikilia nyadhifa zao za umma kwa uwezo wao wenyewe na kwa kustahili kwao, si kwa sababu ya uhusiano wowote na mteja wetu,” sehemu ya barua hiyo inasema.
Pia walitetea rekodi ya Wetang’ula katika utumishi wa umma, wakisema amejenga taaluma yake kupitia bidii na uadilifu alipohudumu katika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo kama Wakili Mwandamizi, mfanyabiashara, kiongozi wa kisiasa na Spika wa Bunge la Kitaifa.

Pia soma
Gachagua adai Ruto amechafua ground Ol Kalou, asema amemwaga KSh 1B kusaka kura: “Chai unalipa na elfu”
Kulingana na mawakili hao, uchapishaji huo ulimweka mteja wao kwenye dharau ya umma, uliharibu sifa yake nchini na kimataifa, na kumsababishia msongo wa mawazo.

Source: Twitter
Wetang’ula anaitaka The Standard ifanye nini?
Miongoni mwa matakwa yake, Wetang’ula anataka The Standard ichapishe kanusho la wazi la habari hiyo kwenye ukurasa wake wa mbele ndani ya saa 48, ichapishe ombi la radhi lisilo na masharti katika toleo linalofuata la gazeti na iondoe makala hiyo kwenye majukwaa yake yote ya kidijitali.
“Kwamba mtoe ombi la radhi la maandishi lisilo na masharti kwa mteja wetu kwenye ukurasa wa mbele wa toleo lijalo la gazeti la The Standard, na kwa vyovyote vile si zaidi ya saa arobaini na nane kuanzia tarehe ya barua hii,” mawakili hao walidai.
Spika huyo pia anataka kukiriwa kwa uwajibikaji ili kufungua njia ya mazungumzo kuhusu fidia, na anataka kampuni hiyo ya habari kusitisha kuchapisha kile anachodai ni taarifa nyingine za kumchafulia jina.
Mawakili wake wameonya kuwa kushindwa kutimiza matakwa hayo ndani ya muda uliowekwa kutamwacha mteja wao bila chaguo lingine isipokuwa kuanzisha kesi za madai na jinai dhidi ya kampuni hiyo ya habari.

Pia soma
Picha: Wetang’ula, Ichung’wah wapokea makaribisho ya kishujaa Eldoret katika mkutano wa UDA
Read: ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
