Mahakama ya Kimataifa ya ICC, imepata mafanikio makubwa kwenye uchunguzi wake wa visa vya uhalifu wa kivita, uliotekelezwa jimboni Darfur nchini Sudan.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Naibu Kiongozi wa mashtaka Nazhat Shameem Khan, ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kuwa, umepokea Ushahidi mwingi na wa uhakika kuhusu vitendo vilivyofanyika kwenye miji ya Al Geneina na Al Fashir mwaka 2023 na 2024.

Aidha, Naibu Kiongozi huyo wa mashtaka wa ICC amesema watalaam wake wametembelea kambi ya wakimbizi Mashariki mwa Chad na kukutana na waathiriwa wa visa hivyo.

Hata hivyo, hakutaja waliohusika moja kwa moja, lakini akaongeza kuwa matokeo yatafahamika hivi karibuni, bila ya kueleza ni lini.

Mauaji makubwa na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilitekelezwa katika miji hiyo, ambayo watalaam wa Umoja wa Mataifa wanasema, wanamgambo wa RSF walitekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya wenyeji ambao hawana asili ya kiarabu.

Sudan sio mwanachama wa ICC lakini Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa lilitoa agizo kwa Mahakama hiyo kuchunguza matukio yte ya uhalifu wa kivita tangu mwaka 2005 na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *