Jeshi la kawaida limepata ushindi mkubwa katika Blue Nile, na pia huko Kordofan na haswa huko Darfur, ngome ya SRF. Mnamo Julai 9, jeshi la serikali ya Sudan lilitangaza rasmi kukamatwa tena kwa mji wa kimkakati wa Kurmuk kwenye mpaka na Ethiopia. Mji huu ulikuwa umeangukia mikononi mwa wananamgambo wa RSF na washirika wao, Vikosi vya Abdelaziz el-Hilu, kufuatia shambulio lao la mwezi Machi mwaka huu.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF yameongezeka katika nyanja zote katika siku za hivi karibuni: huko Kordofan, Blue Nile, na Darfur. Jiji la Kurmuk, huko Blue Nile, lilitekwa tena baada ya saa sita za mapigano makali. Gavana wa mkoa huo alichukua fursa hiyo kuwatolea wito watu 70,000 waliokimbia ghasia mwezi Machi mwaka huu warudi.

Kuhusu Darfur, jeshi linasonga mbele kwa kasi kuelekea jiji la Al-Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi. Jiji hili liliangukia mikononi mwa RSF mwanzoni mwa vita. Wakazi wake, wengi kutoka Massalit, waliuawa. Kumekuwa na majeruhi 15,000 wa raia, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Katika eneo hilo, jeshi limeteka miji ya Abu Srouj, Kulbus, na Jabel Moun, na kwa sasa liko takriban kilomita 50 kaskazini mwa Al-Geneina, ambayo imekuwa moja ya ngome kubwa zaidi za RSF huko Darfur.

RSF ambayo imezidiwa na ambayo iko chini ya shinikizo kuzunguka mji huu, imetuma vikosi vya ziada. Hata hivyo, ngome zao huko Kordofan zililengwa na mashambulizi makubwa na ndege zisizo na rubani za jeshi. Kulingana na Kikosi cha Pamoja cha Washirika, wanajeshi wake 10,000 na vitengo vitatu vya jeshi wanashiriki katika vita hivi.

Mbali na miji michache kwenye mpaka na Chad, majimbo matano ya Darfur yako chini ya udhibiti wa RSF. Mapigano yameongezeka katika eneo hili la mpakani katika siku za hivi karibuni, na maelfu ya raia wamelazimika kukimbia. Jeshi linajaribu kupanua udhibiti wake juu ya maeneo ya mpaka na Chad, Ethiopia, na, baadaye, Libya. Lengo ni kukata njia za usambazaji wa wanamgambo wa RSF.

Kulingana na waangalizi kadhaa, mzozo nchini Sudan umeingia katika awamu mpya. Jeshi, ambalo liko chini ya shinikizo la kimataifa na kukataa mpango wa mjumbe wa rais wa Marekani kwa Afrika, Massad Boulos, ambao linauona kuwa karibu sana na Abu Dhabi, linakataa mapendekezo yake.

Kwa hivyo linatafuta kupiga hatua katika uwanja wa vita ili kupata nafasi ya nguvu. Linategemea kudhibiti njia za usambazaji wa kimkakati ili kuwazuia wanamgambo wa RSF. Pia linatafuta kufungua njia kati ya Kaskazini na Magharibi mwa Darfur, ambayo ingeiruhusu kudumisha uwepo wake. Kwa hivyo, kuikomboa Al-Geneina ndio lengo lake la kimkakati linalofuata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *