Chanzo cha picha, Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2
Tottenham wametoa ofa kwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Randal Kolo Muani, ambaye alitumia muda kwa mkopo huko Spurs msimu uliopita, lakini Juventus, wanasalia kuwa na nafasi ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 27. (Tuttosport – In Itali)
Arsenal wako tayari kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 35 kwa Club Brugge kwa mchezaji wa Ugiriki Christos Tsoliz mwenye umri wa miaka 24 (Sun),
Barcelona wamefungua mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu kusainiwa kwa winga wa Ujerumani Karim Adeyemi, mwenye umri wa miaka 24, na kuibua maswali zaidi kuhusu nafasi ya mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 28 kurudi Nou Camp baada ya mkopo wake. (Sky Germany),
Manchester United inajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Manu Kone, ambaye ana hamu ya kujipima katika Ligi Kuu, pamoja na kwamba Juventus watakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa miaka 25 kwa bei sahihi. (Teamtalk),
Chanzo cha picha, Getty
Liverpool na Arsenal zote ziko tayari kwa kusita kumtoa mkopo kiungo wa kati wa Morocco Ayyoub Bouaddi kurudi Lille ikiwa wanaweza kumsajili msimu huu wa joto, kwani klabu hiyo ya Ufaransa inataka kumbakisha mchezaji huyo wa miaka 18 kwa msimu mmoja zaidi. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood anakaribia kujiunga na Fenerbahce, huku klabu ya Uturuki ikiwasilisha ofa kwa Marseille na wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 24. (Sky Italy)
Crystal Palace na Fulham wanaweza kumsajili kiungo wa kati wa Southampton Ireland Kaskazini Shea Charles, 22, baada ya Leeds kushindwa na ofa mbili. (Sky Sports)
Mchezaji anayelengwa na Manchester United, Aurelien Tchouameni, amejitolea mustakabali wake kwa Real Madrid, huku kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 akitarajiwa kuongeza mkataba wake kwa miaka mitano. Madrid ilikataa kukubali mbinu za United. (AS – In Spanish)
Chanzo cha picha, Getty Images
Nottingham Forest wamefanya mazungumzo na Feyenoord kumhusu beki wa kulia wa timu ya vijana ya Uholanzi chini ya umri wa miaka 21, Givairo Read, mwenye umri wa miaka 20, ambaye pia anafuatiliwa na Manchester City. (Mail)
Klabu ya Torino ya Serie A inaonyesha nia ya kuwasajili kwa mkopo kipa wa Kibrazili wa Leeds United, Lucas Perri (28), na kipa wa Southampton na England, Aaron Ramsdale (28). (Sky Italy}
Brentford na Tottenham zinavutiwa na kiungo mkabaji wa Guinea, Ousmane Diabate (18), na zinaamini zinaweza kumsajili kutoka klabu ya Uturuki ya Genclerbirligi kwa takriban pauni milioni 3 pamoja na marupurupu ya ziada. (Mail),
Coventry wanatarajiwa kumsajili beki wa Uswisi mwenye umri wa miaka 22, Aurele Amenda, kutoka Eintracht Frankfurt kwa dili la thamani ya pauni milioni 17. (Bild Via SportWitness)
Aston Villa wanatarajiwa kusimama imara katika msimamo wao kumhusu kipa wa Argentina, Emiliano Martinez, huku kukiwa na nia endelevu kutoka Juventus ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33. (Birminghamworld)