
Kiongozi wa kiroho wa Iran ​Ayatollah Mojtaba Khamenei ameapa kulipiza kisasi cha mauaji ya babake Ali Khamanei aliyezikwa siku ya Alhamisi, baada ya kuuawa kwenye mashambulizi ya Israeli na Marekani mwezi Februari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu Mojtaba ambaye hakuonekana kwenye mazishi ya babake yake, amesema raia wa Iran wanataka kisasi cha mauaji ya babake kilipizwe.
Trump kwa upande wake ameonya kuwa Iran itaharibiwa kabisa iwapo kutakuwa na jaribio lolote la kumuua.
Vyombo vya habari vya nchini Marekani wiki vilichapisha ripoti kuwa Israeli ilitoa taarifa za kijasusi kwa Trump kuhusu mipango ya Iran kutaka kumuua.
Wakati wa mazishi ya Ali Khamenei, waombolezaji walionekana wakiwa wamebeba mabango yaliokuwa na ujumbe wa kutaka nchi yao kulipiza kisasi cha mauaji yake.