
Jumuiya ya nchi za Madola inataka kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, imalizwe ndani ya siku 30.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jumuiya hiyo imeitaka serikali ya Tanzania kutafuta ufumbuzi wa kisiasa na kisheria kuhusu kesi ya Lissu ambaye amekuwa akizuiwa tangu Aprili mwaka uliopita.
Mapendekezo haya yamewasilishwa na mjumbe maalum wa jumuiya hiyo Lazarus Chakwera, rais wa zamani wa Malawi, ambaye alizuru Tanzania baada ya vurugu za uchaguzi mkuu wa Oktoba wa mwaka 2025.
Mbali na kusuluhisha hatima ya Lissu, mapendekezo ya Jumuiya hiyo, ni kuachiwa huru kwa wafungwa wengine wa kisiasa, hasa waliokamatwa wakati wa machafuko ya kisiasa.
Aidha, serikali ya Tanzania, imetakiwa kurejesha mifumo yote ya kidijitali na kuacha kuwatisha wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu ndani ya siku sitini.
Chakwera ni mpatanishi wa kisiasa nchini Tanzania, kwa lengo la kupatanisha pande hasimu nchini humo kwa kuwezesha mazungumzo ya maridhiano.