Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wametaka viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za chama kuwajibika na kupisha uchunguzi huru, wakisema hatua hiyo itasaidia kurejesha imani ya wanachama na wananchi.

Katibu Mwenezi wa Chadema Jimbo la Newala Mjini, Mkoani Mtwara, Ismail Abdallah Chipalu, amesema anashangazwa na hatua ya chama kuwafukuza uanachama au kuwachukulia hatua wanachama wanaohoji tuhuma hizo badala ya kutoa majibu ya kina kuhusu matumizi ya fedha zinazolalamikiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Newala, Chipalu amesema alitarajia viongozi wa chama wangeitisha kikao cha kujadili hoja zilizotolewa na wanachama badala ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanaozibua.

“Kwa mfumo huu najiuliza tutafukuza wanachama wangapi? Viongozi wa juu wanatutegemea sisi wa chini kuendelea kuwajengea chama na kuwaleta wanachama wapya,” amesema.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Kibaha, Shabani Mchezo.

Amesema viongozi wa kitaifa wamekuwa hawafiki mara kwa mara katika majimbo, jambo linalowaacha viongozi wa ngazi za chini wakikabiliwa na maswali ya wanachama bila kuwa na majibu ya kuridhisha.

Chipalu amesema suluhisho si kuwachukulia hatua wanaoibua hoja, bali ni kuweka wazi taarifa za mapato na matumizi ya fedha za chama ili kuondoa sintofahamu.

Kwa upande wake, Katibu wa Chadema Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi, Zidadu Matila, amesema viongozi wa ngazi za chini wanapata wakati mgumu kuwajibu wanachama kuhusu tuhuma hizo.

Amesema kwa kuwa Chadema imekuwa ikijinasibu kuwa kinara wa uwajibikaji na uadilifu, viongozi wanaotuhumiwa wanapaswa kupisha uchunguzi hadi ukweli utakapobainika.

“Uchunguzi ukifanyika na ukweli ukajulikana, hatua stahiki zichukuliwe. Tunatarajia viongozi wanaotuhumiwa watazungumza na umma kwa ushahidi na uwazi,” amesema.

Matila amesema chama hakiwezi kuendelea kukosoa ubadhirifu wa fedha serikalini huku kikishindwa kujibu tuhuma zinazokikabili, hali ambayo inaweza kupunguza imani ya wananchi.

Pia amegusia suala la, akisema harakati za chama zimeonekana kudhoofika tangu kiongozi huyo alipowekwa kizuizini, na kuomba mamlaka husika pamoja na uongozi wa chama kutafuta suluhu ili aweze kuendelea na shughuli zake za kisiasa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema Mkoa wa Pwani, Shabani Mchezo, amemtaka kujitokeza hadharani kuelezea tuhuma zinazozungumzwa kuhusu fedha za chama.

Amesema ukimya wa viongozi wakuu unaweza kuendelea kukichafua chama mbele ya umma, hivyo ni muhimu kutoa maelezo ya wazi ili kuondoa mashaka yaliyopo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *