Mawaziri wa mambo ya nje toka nchi za G7 na umoja wa Ulaya, wametoa wito kwa wapiganaji wa RSF nchini Sudan pamoja na washirika wake, kuacha mara moja kutekeleza operesheni za kijeshi kwenye mji wa El Obeid.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yao, mawaziri hayo wamelitaka Kundi hilo kuepuka shughuli zozote ambazo huenda zikasababisha kutokea kwa mauaji ya halaiki au kuhatarisha maisha ya rai awa eneo hilo.

Aidha wamezitaka pande zinazohasimiana, likiwemo jeshi la Serikali, kusitisha mapigano, kushiriki mazungumzo jumuishi na kwakuaminiana Pamoja na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wenye uhitaji.

Mawaziri hao wameunga mkono azimio la umoja wa Mataifa linalotaka pande hizo kukomesha vita Pamoja na kulitaka baraza la usalama kuongeza muda makataa ya vikwazo vya silaha kwenye jimbo la Darfur.

Haya yanajiri wakati huu waendesha mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC, wakipendekeza kwa majaji wa mahakama hiyo kuondoa mashtaka dhidi ya kiongozi wa zamani wa waasi wa Sudan, Abdallah Banda, aliyeshtakiwa kwa tuhuma za kuhisika na shambulizi dhidi ya walinda amani wa umoja wa mataifa mwaka 2007.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *