
Nchini Senegal, rais wa zamani Macky Sall, anatarajiwa jijini Dakar hivi leo, anakotarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mrithi wake Bassirou Diomaye Faye. Sall, anawania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii ni mara ya kwanza kwa Sall kurejea nchini Senegal, baada ya kuondoka Aprili 2024 wakati chama chake kiliposhindwa kwenye uchagazi mkuu.
Waziri wa Ulinzi Yankhoba Diémé, amesema rais huyo wa zamani yupo huru kurejea nchini Senegal, na hakuna njama yoyote ya kumkamata na kumfungulia mashtaka kuhusu tuhma za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa utawala wake.
Wachambuzi wa siasa wanasema, rais Faye na mtangulizi wake wanakutana kwa sababu ya maslahi ya kisiasa. Mack Sall, anataka Senegal iunge mkono mpango wake wa kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Faye naye yupo kwenye mchakato wa kutafuta washirika wapya wa kisiasa baada ya kutofautiana na aliyekuwa mshirika wake Ousamane Sonko, na hivyo anataka uungwaji mkono wa wafuasi wa Sall ili kuanza kujiandaa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2029.
Tayari chama cha Sall cha APR kinaonekana kuungana na Faye, ambaye anapanga kuunda muungano mpya wa kisiasa.