Raia kadhaa wa Marekani waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya virusi vya Ebola nchini DRC kwa sasa wako karantini katika kituo kimoja nchini Kenya, kinachoendeshwa na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Marekani. Taarifa hii ilithibitishwa kwa RFI siku ya Ijumaa, Julai 17, 2026, na afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo iliielezea kama “hatua ya tahadhari.”

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Albane Thirouard

Washington inawataka raia wake ambao wamekuwa DRC kujitenga kwa siku 21 katika nchi ya tatu kabla ya kurudi Marekani. Hata hivyo, mahakama za Kenya zimesimamisha ufunguzi wa kituo hiki  cha Marekani nchini Kenya.

Shirika lisilo la kiserikali la Marekani la Samaritan’s Purse, linalohusika katika mapambano dhidi ya virusi vya Ebola nchini DRC, pia limethibitisha kwamba wanachama saba wa Marekani wa timu yake kwa sasa wako karantini kwa siku 21 katika kituo cha Marekani nchini Kenya. Kulingana na Mkurugenzi Mkuu shirika hilo, Franklin Graham, wamewekwa katika mahema makubwa ya kijeshi ndani ya eneo lenye uzio, wakilala kwenye vitanda vinavyokunjwa na kubebeka kwa urahisi na kupewa chakula na jeshi la Marekani.

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambaye alithibitisha taarifa hiyo kwa RFI, alibainisha kuwa raia hawa wa Marekani hawakuwa na dalili zozote za maambukizi ya virusi vya Ebola na walipimwa na hawakukutwa na virusi hivyo. Uhamisho wao kwenda Kenya, kulingana na chanzo hiki, ni “hatua ya tahadhari.”

Waziri wa Afya wa Kenya “hana taarifa hii”

Wafanyakazi wa misaada wanafuatiliwa na madaktari kutoka Huduma ya Afya ya Umma ya Marekani, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo ilisema kwamba mamlaka ya Kenya iliidhinisha uhamisho wao kwenda kituo cha Marekani. Waziri wa Afya wa Kenya Aden Duale aliliiambia shirika la habari la AFP kwamba “hana taarifa hii”.

Tangazo la mwezi Juni kwamba Washington ilikuwa ikijenga kituo cha karantini cha wagonjwa wa Ebola nchini Kenya kwenye kambi ya jeshi la wanahewa katikati mwa Kenya ili kuwahifadhi raia wake ambao wanaweza kuwa katika hatari ya kuambukizwa virusi vya Ebola lilizua hasira na kusababisha maandamano, ingawa hakuna kesi zilizoripotiwa nchini Kenya. Mahakama zilisimamisha mradi huo, na Waziri wa Afya alithibitisha mahakamani kwamba aliamuru kusitishwa kwake.

Hata hivyo, vyombo kadhaa vya habari vilikuwa tayari vinaripoti wakati huo kwamba maandalizi yalikuwa yakiendelea. Mnamo mwezi Juni, watu watatu waliuawa wakati wa maandamano dhidi ya mpango wa kituo hiki cha karantini cha Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *