Jeshi la Iran lafanya mashambulizi mapya ya droni katika kambi za Marekani huko Kuwait/IRGC yatungua droni ya MQ-9 huko Ahvaz

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumapili, jeshi la Iran limeeleza kuwa mashambulizi hayo yalianza mapema leo ikiwa ni jibu kwa hatua ya Marekani ya kukiuka mikataba ya kimataifa na kuendesha mashambulizi dhidi ya maeneo ya raia.

 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege zisizo na rubani za Iran (droni) zimeshambulia ghala la silaha la Marekani katika kambi ya kijeshi ya Buehring (ambayo zamani ilijulikana kama kambi ya Udairi) pamoja na maeneo ya kuhifadhia vifaa na makao ya askari katika Kambi ya Jeshi la Anga ya Ali Al Salem nchini Kuwait.

Jeshi la Iran limebainisha kuwa maeneo hayo yote mawili yameshambuliwa kwa mara ya pili.

Taarifa ya jeshi la Iran imesisitiza kuwa kampeni ya kijeshi ya nchi inalenga kulinda utambulisho wa taifa, historia ya karne nyingi, na watu wake ambao, kwa kuzingatia kanuni za Kiislamu hawatendi dhulma wala hawasalimu amri mbele ya dhulma na ukandamizaji.

Mapema leo, jeshi la Iran liliarifu kuwa limeshambulia ghala za silaha za jeshi la kigaidi la Marekani katika Kambi ya Udairi, pamoja na rada ya Patriot na rada ya anga ya jeshi la Marekani katika kambi ya Ali Al-Salem nchini Kuwait, kupitia mashambulizi makali ya ndege zisizo na rubani zenye uwezo mkubwa wa uharibifu na maangamizi.

Wakati huo huo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC leo limetangaza kuwa limeizuia na kuisambaratisha droni ya adui aina ya MQ-9 katika mji wa Ahvaz kuisni magharibi mwa Iran.

IRGC imetangaza kuwa leo Jumapili imetungua ndege isiyo na rubani ya aina ya MQ-9 katika anga ya mji wa Ahvaz.

Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imearifu kuwa ndege hiyo isiyo na rubani aina ya MQ-9 ilitunguliwa na mfumo mpya wa ulinzi wa anga unaoendeshwa na Kikosi cha Anga cha IRGC.

Msemaji wa Makao Makuu ya Khatamal-Anbiya ya ameionya Marekani kwamba Iran italenga miundo mbinu iliyosalia katika kanda hii iwapo miundombinu yake ya ndani itashambuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *