Chanzo cha picha, Edwin Remsberg / VWPics/Universal Images Group via Getty Images)
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 6
Takriban watalii milioni 307 walisafiri nje ya nchi katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, idadi ambayo ni kubwa kwa takriban milioni sita ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2025, kulingana na takwimu kutoka Shirika la Utalii Duniani (UNWTO).
Hii ni ongezeko kubwa linalothibitisha ubora wa mwaka 2025, ambapo idadi ya watalii wa kimataifa ilifikia bilioni 1.52—kiasi kinachozidi takwimu za mwaka 2024 kwa takribani milioni 60.
Barani Afrika, idadi ya watalii walioingia iliendelea kuongezeka katika robo ya kwanza ya mwaka 2026 (+4%), huku kanda ya Afrika Kaskazini ikiongoza kwa ongezeko la asilimia 18 (+18%). Idadi ya watalii walioingia katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara pia iliongezeka kwa takriban asilimia nnw katika robo hiyo ya kwanza.
Chanzo cha picha, Nick Dale/Design Pics Editorial/Universal Images Group via Getty Images)
Kwengineko duniani Ulaya iliwapokea watalii wa kimataifa milioni 130 katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na kipindi sawia na hicho mwaka uliopita, huku Asia na eneo la Pasifiki zikishuhudia ukuaji wa asilimia tatu na Amerika asilimia mbili, kulingana na UNWTO.
Baada ya kuongezeka mwezi Januari na Februari, idadi ya wageni wa kimataifa katika Mashariki ya Kati ilishuka kwa asilimia 37, kutokana na athari za vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Ukuaji uliorekodiwa katika robo ya kwanza unathibitisha kuimarika kwa kasi kwa sekta ya utalii duniani, hali iliyoonekana tangu kipindi cha baada ya janga la COVID-19.
Maeneo makuu yanayovutia utalii yanaendelea kuwa Ulaya, ikiwa na watalii wa kimataifa milioni 793 mwaka 2025; Amerika ikiwa na milioni 218; Asia-Pasifiki ikiwa na milioni 331; Mashariki ya Kati ikiwa na wageni wa kimataifa milioni 100; na Afrika—ikiwa na vivutio mbalimbali, safari za kujinea wanyamapori, urithi wa kitamaduni, maeneo ya kihistoria na fukwe zenye jua—ambayo imevutia takriban watalii milioni 81 mwaka 2025.
Kwa mujibu wa UNWTO, jumla ya mapato yatokana na mauzo ya huduma za utalii (ikiwemo mapato ya usafirishaji wa abiria na huduma nyingine za usafiri) yanakadiriwa kufikia dola za Marekani trilioni 2.2 mwaka 2025.
Hizi hapa ni nchi 10 bora barani Afrika zinazovutia idadi kubwa zaidi ya watalii wa kimataifa.
1. Morocco
Chanzo cha picha, Jakub Porzycki/NurPhoto via Getty Images
Morocco imekuwa kivutio kikuu cha watalii barani Afrika, mamlaka nchini humo ulitarajia kuwapokea takribani watalii milioni 20 kufikia mwaka wa 2025.
Idadi ya watalii wanaowasili nchini Morocco imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka kumi, ikipanda kutoka milioni 10 mwaka wa 2015 hadi milioni 19.8 mwaka wa 2025, kulingana na takwimu rasmi kutoka ufalme huo.
Nchi hiyo imelipiku taifa la Misri, ambalo hapo awali liliongoza katika viwango hivyo. Mafanikio haya yanatokana na sera inayolenga kuiunganisha nchi hiyo na masoko muhimu ya utalii kupitia usafiri wa anga.
Masoko makuu ya asili ya watalii yanaonyesha matokeo yanayodhihirisha mvuto wa Ufalme wa Morocco kwa watalii: Ufaransa (+11%), Uhispania (+12%), Uingereza (+18%), Ubelgiji (+10%) na Italia (+21%), kulingana na takwimu rasmi kutoka Ufalme huo.
Sekta ya utalii sasa inachangia asilimia 7.3 ya Pato la Taifa (GDP) la Morocco na kuingiza mapato ya takribani dirham bilioni 124 sawa na (euro bilioni 11.5).
2. Misri
Chanzo cha picha, Jakub Porzycki/NurPhoto via Getty Images)
Misri ilipokea watalii milioni 19 mwaka 2025, ongezeko la asilimia 21 ikilinganishwa na mwaka 2024, kulingana na takwimu kutoka kwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Sherif Fathy.
Waziri Fathy alisisitiza “ushindani wa Misri kama eneo salama la kutembelea, pamoja na mafanikio ya mkakati wetu wa kutoa bidhaa mbalimbali za utalii huku tukiimarisha ubora wa huduma.”
Kama uthibitisho kwamba utalii una uhusiano mkubwa na usafiri wa anga, idadi ya safari za ndege za kukodi nchini humo iliongezeka kwa asilimia 32.
Mamilioni ya wageni bado huvutiwa na maeneo maarufu kama vile piramidi za Giza, mahekalu ya Luxor na Jumba la Makumbusho la Grand Egyptian, ambalo lilifunguliwa mwaka 2025.
Serikali ya Misri imeweka lengo la kuongeza idadi ya watalii wa kigeni kufikia milioni 30 kwa mwaka ifikapo mwaka 2028.
Sekta ya utalii ilichangia takriban dola bilioni 15.3 katika uchumi wa taifa mwaka 2024, kulingana na takwimu rasmi.
3. Tunisia
Chanzo cha picha, Imen Ben Youssef / Hans Lucas / AFP via Getty Images
Tunisia imesalia kuwa kivutio kikubwa cha utalii barani Afrika. Ingawa bado iko nyuma sana ikilinganishwa na Morocco na Misri, nchi hiyo ilivuka kizingiti cha watalii milioni 11 kufikia mwaka wa 2025, kulingana na Waziri wa Utalii, Bw. Sofiane Tekaya.
Tunisia, ambayo katika miaka ya hivi karibuni imejikita katika miradi ya kufufua sekta hiyo kwa kupanua wigo wa huduma na vivutio vyake vya utalii, inatarajia kufikia viwango vya juu zaidi katika miaka ijayo.
4. Afrika Kusini
Chanzo cha picha, Per-Anders Pettersson/Getty Images
Nchi hii inaendelea kuwa kivutio maarufu cha watalii wa kimataifa kutokana na mbuga na mandhari yake ya kupendeza,
Mwaka wa 2025, nchi hiyo ilikaribisha wageni milioni 10.48 wa kimataifa, ongezeko la 17.6% ikilinganishwa na mwaka wa 2024 na rekodi kamili kulingana na Wizara ya Utalii.
Katika hamu yake ya kuifanya sekta hiyo kuwa kipaumbele katika suala la uzalishaji wa utajiri na uundaji wa ajira, serikali ya Afrika Kusini imeidhinisha Mpango wa Ushirikiano wa Ukuaji wa Utalii.
Mwisho unalenga kuboresha ufikiaji wa wasafiri, kupitia kuanzishwa kwa idhini ya usafiri wa kielektroniki (eTA) katika masoko muhimu, na kuimarisha muunganisho wa nchi miongoni mwa mambo mengine.
Mwaka wa 2024, utalii ulichangia dola bilioni 9 kwa uchumi wa Taifa la Upinde wa Mvua.
5. Kenya
Chanzo cha picha, SIMON MAINA/AFP via Getty Images)
Katika kanda ya Afrika Mashariki, Kenya inaendelea kuwa kivutio kikuu cha watalii. Kulingana na Waziri wa Utalii na Wanyamapori Rebecca Miano, nchi hiyo ilipokea wageni milioni 7.9 mwaka wa 2025, ikilinganishwa na milioni 7.6 mwaka uliotangulia.
Mwaka wa 2025, sekta ya utalii ya Kenya iliingiza mapato ya shilingi bilioni 500 (takriban dola bilioni 3.84), kiasi ambacho ni asilimia 10 zaidi ya mapato ya mwaka wa 2024.
Ili kurahisisha mtiririko wa watu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, mamlaka zilitangaza kuondolewa kwa hitaji la kibali cha kielektroniki cha kusafiri kwa raia wa nchi za Afrika; aidha, Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) ilizindua kampeni ya kimataifa mwezi Mei mwaka jana yenye kichwa “A Journey Through the Wild Heart of East Africa,” kwa ushirikiano na BBC StoryWorks.
6. Tanzania
Chanzo cha picha, Nick Dale/Design Pics Editorial/Universal Images Group via Getty Images)
Tanzania ni kivutio kikubwa cha utalii Afrika kutokana na mbuga zake nyingi na wanyamapori wa kipekee wanaonaendelea kuwavuwatia mamilioni ya watalii wa kimataifa. Kufikia mwaka 2025, watalii milioni 5.9 walikuwa wametembelea nchi hiyo.
Sasa Tanzania inalenga kufikisha idadi ya watalii milioni 8 ifikapo mwaka 2030 na kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika Pato la Taifa (GDP) kutoka asilimia 17 hadi asilimia 20.
Sekta hiyo iliingizia uchumi wa Tanzania takriban dola bilioni 4.2, kulingana na takwimu rasmi.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi