
Nchi za Umoja wa Ulaya hatimaye zimefikia makubaliano leo Alhamisi asubuhi huko Brussels ya kuiwekea Urusi vikwazo vipya, wanadiplomasia wamesema, baada ya wiki kadhaa ndefu za mazungumzo na hatua za vikwazo kutelekezwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kifurushi hiki cha 21 cha vikwazo, kilichopatikana Alhamisi asubuhi baada ya mazungumzo magumu, kinalenga hasa kuongeza kwa mwaka mwingine kikomo cha bei kwa mauzo ya nje ya mafuta ya Urusi, kwa dola 44 kwa pipa. Hii inapunguza mapato ya mafuta ya Urusi, ambayo yanafadhili sehemu kubwa ya vita vyake dhidi ya Ukraine. Hili ni muhimu zaidi kwa sababu, bila kuongezwa kikomo hiki cha bei, mafuta ya Urusi yangeweza kuuzwa kwa bei zinazokaribia zile za soko la kimataifa, ambazo ni kubwa kutokana na vita nchini Iran.
Kifurushi cha vikwazo vilivyojadiliwa na kupunguzwa
Kifurushi hik ikipya cha vikwazo, matokeo ya wiki za mazungumzo, ilibidi kipunguzwe ikilinganishwa na pendekezo la awali la Brussels. Hasa, ilibidi ibadilishwe ili kushughulikia wasiwasi wa Ugiriki kuhusu gesi asilia iliyoyeyushwa ya Urusi (LNG). Athens ilitaka EU iruhusu kampuni zake kuendelea kusafirisha LNG, mradi tu imekusudiwa kwa wateja nje ya Ulaya. Makubaliano yamefikiwa kuhusu hatua hii. Uhamisho huu wa LNG kwenda nchi za tatu utaidhinishwa kwa msamaha maalum kwa mikataba iliyohitimishwa kabla ya Februari 24, 2022, tarehe ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Nchi za Ulaya zitapitia upya msamaha huu kila mwaka.
Hatua zingine zimeachwa au kulegezwa. Tume ya Ulaya ilikuwa imependekeza kuwapiga marufuku Warusi waliopigana nchini Ukraine kuingia Umoja wa Ulaya. Kulingana na wanadiplomasia, nchi wanachama zimejitolea tu kufanya kazi kuelekea marufuku kama hiyo katika siku zijazo. Bulgaria pia ilijivunia kufanikiwa kuzuia kuingizwa kwa kiongozi wa Kanisa la Orthodox kutoka Urusi Kirill kwenye orodha ya watu walio chini ya kuzuiwa mali na marufuku ya visa. Wanadiplomasia pia wameonyesha kwamba Ureno na Ufaransa zilipinga kukomeshwa kwa uagizaji wa chewa wa Urusi.
“Vikwazo vyetu vinaendelea kudhoofisha ufadhili wa vita ya Urusi”
Kifurushi hiki cha vikwazo pia kinajumuisha marufuku ya miamala inayolenga sekta ya fedha ya Urusi, pamoja na hatua mpya dhidi ya sarafu za kidijitali. Pia inalenga meli mpya za mafuta zinazotumiwa na Urusi chini ya bendera za uwongo kusafirisha nishati na bidhaa zingine. Hatimaye, inajumuisha vikwazo vipya vya biashara ili kudhoofisha tasnia ya kijeshi ya Urusi.
“Wakati ambapo Ukraine inapiga hatua katika upande wa kijeshi, vikwazo vyetu vinaendelea kudhoofisha ufandhili vita ya Urusi,” Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X.