- Aliyekuwa gavana wa Nairobi Anne Kananu alihama rasmi chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Rais William Ruto siku ya Jumatano, Julai 22
- Kananu alijiunga na National Economic Development Party (NEDP) kinachoongozwa na aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko
- Anatarajiwa kuwania kiti cha ubunge cha Eneo Bunge la Mara katika Kaunti ya Tharaka Nithi kwa tiketi ya NEDP katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027
Aliyekuwa gavana wa Nairobi Anne Kananu ameondoka katika chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Rais William Ruto na kujiunga rasmi na National Economic Development Party (NEDP) kinachoongozwa na mtangulizi wake, Mike Sonko.

Source: Facebook
Sonko alitangaza kujiunga kwa Kananu na chama hicho usiku wa Jumatano, Julai 22, akifichua kuwa analenga kuwania kiti cha ubunge cha Eneo Bunge la Mara katika Kaunti ya Tharaka Nithi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Kananu ahamia NEDP
“Leo tunamkaribisha kwa fahari Anne Kananu ndani ya NEDP baada ya kuhama rasmi kutoka UDA. Atawania kiti cha ubunge cha Eneo Bunge la Mara katika Kaunti ya Tharaka Nithi kwa tiketi ya NEDP. Kwa pamoja, tumejitolea kupambana na umaskini, kuboresha miundombinu, kuunda nafasi za kazi, kupanua upatikanaji wa elimu bora na maji safi, na kurejesha matumaini kwa wananchi wa Mara. Karibu NEDP, Anne Kananu. Mustakabali uko hapa,” alisema Sonko.
Kuondoka kwa Kananu kutoka UDA kunachukuliwa kuwa mabadiliko muhimu ya kisiasa, huku chama hicho kikiendelea kuwa nguzo kuu ya utawala wa Rais Ruto kuelekea duru ijayo ya uchaguzi.
Sonko atoa onyo kuhusu uteuzi wa chama
Licha ya shamrashamra zilizozunguka kuhamia kwa Kananu NEDP, Sonko alisisitiza kuwa uanachama wa chama hicho hauhakikishi mtu kupata tiketi moja kwa moja.
Alisema wote wanaotaka kugombea, akiwemo Kananu, watalazimika kutafuta uungwaji mkono wa wananchi kupitia mchujo wa ushindani ndani ya chama.
“Kila anayewania nafasi lazima aende kwa wananchi, apate uungwaji mkono wao na ashindane kwa haki katika mchujo wa chama chetu. NEDP inaamini katika uteuzi wa huru, wa haki na wa kidemokrasia,” alisema Sonko, akiongeza kuwa kupiga picha naye au kujiunga na chama hakutampa mtu yeyote tiketi ya moja kwa moja.

Source: Facebook
Historia ya kisiasa ya Kananu
Kananu alihudumu kama gavana kamili wa Nairobi kuanzia Novemba 2021 hadi Agosti 2022.
Aliingia madarakani baada ya Mike Sonko kuondolewa ofisini kupitia mchakato wa kumng’atua.
Alikamilisha kipindi kilichosalia cha muhula wa ugavana wa 2017 hadi 2022 kabla ya kukabidhi ofisi kwa Johnson Sakaja, aliyeshinda uchaguzi wa ugavana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.

Pia soma
Mbunge wa EALA Kanini Kega Asema Amenyang’anywa Walinzi Mara Baada ya Uchaguzi Mdogo wa Ol Kalou
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Chanzo: TUKO.co.ke
