KATIBU Mkuu wa Mlandege, Hussein Ahmada amesema dirisha hili kubwa la usajili wameacha wachezaji 15 lakini wana mpango wa kusajili wengine kwa lengo la kukijenga kikosi chao upya.

Kiongozi huyo amesema wachezaji hao wameshawapa barua, pia kuna waliowauza na waliomaliza mikataba.

Hussein amesema, wachezaji walioachwa na waliouzwa idadi yao inafika 15 hadi sasa na hakuna mabadiliko yoyote, kilichobaki sasa ni kuanza kutambulisha majembe mapya.

“Tunataka kutengeneza timu yetu upya, kwa hiyo tutasajili wachezaji wenye uzoefu na uwezo ambao watakwenda na kasi ya Mlandege na si vinginevyo,” amesema.

Katibu huyo amesema, uongozi umeanza mchakato wa kukijenga upya kikosi chake kuelekea msimu mpya baada ya kuwaacha wachezaji 15 katika dirisha kubwa la usajili.

Amesema, uongozi wa klabu tayari umeanza kusajili wachezaji wapya watakaongeza ushindani ndani ya kikosi, huku utambulisho wao ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *