Uhispania inakabiliwa na milipuko kadhaa ya moto wa nyika kwa wakati mmoja, ikiwa ni pamoja na milipuko kadhaa nje kidogo ya mji mkuu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uhispania imetangaza hali ya dharura ya kitaifa mjini Madrid na mkoa wa Avila, karibu na mji mkuu, kufuatia milipuko kadhaa ya moto wa nyika inayoteketea bila kudhibitiwa.

Kwa ujumla, zaidi ya watu 10,000 wamehamishwa kutoka maeneo mbalimbali ya Madrid katika siku za karibuni, huku mioto kadhaa ya misituni ikiendelea kuwaka kwa wakati mmoja katika eneo hilo.

Karibu hekta 125,000 za ardhi tayari zimeteketea kwa moto nchini humo mwaka huu.

Milipuko hiyo ya moto inachochewa na upepo na wimbi la joto, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kuhama. Hali ya hatari imetangazwa katika eneo la Madrid, ambapo zaidi ya hekta 130,000 tayari zimeteketea tangu mwanzo wa kiangazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *